Christian
Churches of God
[134]
Yoshua, Masihi,
Mwana wa Mungu
(Toleo La 3.0 19950909-20000219)
Jarida hili linaelezea kuhusu ni nani
anayepasaswa kuabudiwa kwamba ni Eloa. Mwana ambaye alikuwa ni elohim wa
Israeli na Yoshua Masiahi ananyeshwa kwenye muktadha sahihi wa kibiblia.
Matumizi ya jina Yoshua kwenye Biblia kumeelezewa na kuainishwa pia.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki Hati © 1995, 1996, 1998, 2000 Wade Cox)
(Tr.
2017)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa
kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na
anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna
malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala
yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo
zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya
sheria ya haki miliki.
Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti
yetu ya:
http://www.logon.org and http://www.ccg.org
Yoshua, Masihi, Mwana
wa Mungu
Kumbukumbu la Torati
6:4-5 Sikiza, Ee
Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe
mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa
nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa
katika moyo wako
Andiko hili ni Shama au Shâma´ (SHD
8085). Jina lenyewe limechukuliwa kutoka kwenye neno Shama linalomaanisha kusikia ambalo ni neno la kwanza kwenye andiko hili. Ukanunishaji
wan eno kusikia maana yake ni kusikia na kuelewa. Man no yenyewe
yamechanganyika kati ya Kirumi na Kiebrania:
Shama Y’srael Jehovah Elohinu Jehovah Ehad
Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu
wetu, Bwana ndiye mmoja.
Neno Mungu
lililotumiwa kwenye tafsiri ya Kiingereza God
limeeleweka kwa ujumla kama lilivyotafsiriwa kwenye kamusi ya SHD 430 elohim.
Hatahivyo, elohim ni neno la uwingi, ambalo laweza kutumika pia kwenye umoja.
Neno la umoja katika kumtaja Mungu na neno lililosahihi zaidi linalofanana au
kuhusiana na neno hili ni la umoja Eloah.
Andiko lililo kwenye Kumbukumbu la Torati 6:5 linaenda mbali zaidi kwa kutumia
kijisarufi chanya kwenye jina Yehovah Eloheik lenye
maana ya Bwana Mungu wako. Kumbukumbu
la Torati 6:3 inatumia neno YYehovah Elohi kama Mungu wa Mababa. Haya ni
maandiko yanayomtaja kiumbe mmoja lakini Elohi anaonenaka kwa kisarufi cha
uwingi. Elohim ni neno la uwingi. Eloah ni neno la
umoja linaloonyesha kuwa hakuna uwingi. Eloah ni
Mungu Baba kutokana na Mithali 30:4-5 aliye na mwana. Wale wateule wanao lijua
hilo wanaweza kulitangaza jina lake.
Mungu huyu, Eloah, ni Mungu Aliye Juu Sana. Mungu
huyu Aliye Juu Sana hakai kati ya watu (Matendo 7:48). Sisi tu watumishi wa
Mungu Aliye Juu Sana (Matendo 16:17) ambaye ameonyeshwa na kutambulishwa kwenye
Agano la Kale kama Mungu wa Mababa wa Imani. Hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu
huyu wala kumsikia sauti yake (Yohana 1:18; 1Timotheo 6:16).
Jina la Bwana kwenye Agano la Kale ni Eloah. Ezra
anaonyesha kwamba Eloah ni Mungu wa Hekalu, ambaye nyumba ile ya ibada
iliwekwa wakfu kwake. (Ezra 6:16-17), na ndiye aliyekusudiwa kuabudiwa humo
(Ezra 4:24; 5:1-2,5,8,13-16; 6:7-8) huko Yerusalemu (Ezra 5:17;
6:5). Eloah ni Mungu wa mbinguni na duniani (Ezra 5:11; 6:9). Dhabihu
zinatolewa kwa Eloah wa mbinguni (Ezra 6:3, 10). Alikuwa ni huyu Eloah
aliyesababisha jina lake likae huko
Yerusalemu (Ezra 6:12). Makuhani wamepangiwa kwenye maeneo yao chini ya kuhani
mkuu na Walawi kwenye maeneo yao waliyopangiwa kuhudumu ili kumtumikia
Eloah (Ezra. 6:18) (soma pia jarida la Mungu Tumuabuduye (Na. 002)).
Eloah ni Mungu aliye Muumbaji na ni Mwamba wa
wokovu. Yeshuruni alimtafuta Eloah aliyemuumba na alikuwa ni Mwamba wa
wokovu wake (Kumbukumbu la Torati 32:15) na alitoa dhabihu kwa mapepo ambao
hawakuwa Eloah au walengwa stahiki wa kuabudiwa (Kumbukumbu la Torati
32:17). Ni Eloah peke yake ndiye anayestahili kuabudiwa mle Hekaluni.
Ndiye anayestahili anayeonekana kuwahudumia Wana wa Mungu kwenye kitabu cha
Ayubu. Jina Eloah linajitokeza mara 45 kwenye kitabu cha
Ayubu. Eloah hajawahi kuwa na makala (ingawaje limeandikwa kwa
kisarufi kwenye Habakuki 1:11, na linaonekana mara moja tu kwenye auandishi wa
Zaburi 114:7; Marvin H Pope El in the Ugaritic Texts;
soma pia ‘eloah, R. Laird Harris et al., Theological
Wordbook of the Old Testament, Moody Bible Institute, Chicago, 1980, p. 43).
Eloah halijawahikuonekana likijumuishwa na jina linguine takatifu (ibid.).
Eloah anajulikana na kuonyeshwa kama Mungu
aliyefunuliwa kwenye Kutoka 34:6-7 kama tunavyoona kutokana na matumizi yake
kwenye Nehemia 9:17.
Kutoka 34:6-7 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu
mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na
kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu
elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu
mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na
wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
Kwa hiyo Yahova aliyekuwa akipita mbele ya Musa
akimtangaza El ambaye alijulikana kuwa ni Eloa alikuwa Mungu.
Nehemia 9:17 ila wakakataa kutii, wala
hawakuyakumbuka maajabu yako, uliyoyafanya kati yao; lakini wakafanya shingo
zao kuwa ngumu, na katika kuasi kwao wakaweka jemadari, ili wairudie hali ya
utumwa; lakini wewe u Mungu, uliye tayari kusamehe, mwenye neema, mwenye huruma
nyingi, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, basi hukuwaacha.
Danieli 11:37-39 inaonyesha kuwa mpingamungu mkuu alikuwa
mungu au eloah, aliyejiimarisha mwenyewe. Kwa hiyo Eloah anaonekana kama
Mungu sahihi na anayefaa na kustahili kutumainiwa. Jina Eloah lina
maana sawa tu na jina Elah[h] jina analoitwa \Mungu kwa Kiaramu
kilichotumika kwenye biblia. Mungu huyu ni Mkuu na Muweza kama tunavyoona
alivyotumika kwenye Ayubu. Eloah ni msingi au chimbuko la
jina la All’ah wa Waislamu.
Jina Eloah limejitokeza mara tatu kwa sambamba na
neno mwamba kama neno lisiloloelezeka
kuhusu Mungu (Kumbukumbu la Torati 32:15; Zaburi 18:31 [H 32]; Isaya 44:8). Kwa
ujumla, kwa uchache Eloah limetumika mara tatu kwa muktadha wa utisho
kwa wenye dhambi (Zaburi 50:22; 114:7; 139:19). Mlengwa akiwa ni Eloah,
Baba, alikuwa ndiye muumbaji na anayeuongoza na kuufanya uwepo ulimwengu
(Mwanzo 1:1; Nehemia 9:6; Zaburi 124:8; Isaya 40:26,28; 44:24; Matendo 14:15;
17:24-25; Ufunuo 14:7). Kwa utashi wake vitu vyote vilumbwa na kuwepo.
Ufunuo 4:8-11 Na hawa wenye uhai
wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho,
wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,
Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja. 9 Na hao wenye uhai
wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani,
yeye aliye hai hata milele na milele, 10 ndipo hao wazee ishirini na wanne
huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye
aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha
enzi, wakisema, 11 Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu
wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba
vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
Mlengwa huyu kwenye ibada ya Mwanakondoo na baraza la
Wazee ni Mungu ambaye ndiye Baba. Baraza la Wazee ni serikali ya
mbinguni ya Mungu.
Mungu kabla ya mwanzo
Mungu alikuwepo na aliishi peke yake kabla ya kiukmbe
kingine chochote. Alikuwa peke yake kabla ya mwanzo wa uumbaji. Hivyo, ni yeye
peke yake ndiye alikuwepo kabla ya kuwepo kwa vitu vote.
Isaya 43:10 Ninyi ni mashahidi wangu,
asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu
ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu
mimi hatakuwapo mwingine.
Kabla ya yeye hakuna El aliyekuwepo wala aliyeumbwa na
wala hatakuwepo mwingine baada ya yeye na aliye kama yeye. Kwa hiyo, yeye ni wa
Kwanza na wa Mwisho, Alfa na Omega. Kutokana na Ufunuo 1:8, ufunuo ambao Mungu
alimpa Yesu Kristo, Mungu anamwambia Kristo kwamba yeye ni Alfa na Omega na ni
Mwenyezi.
Ufunuo 1:8 Mimi ni Alfa na Omega,
mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja,
Mwenyezi.
Hivyo basi, Baba akiwa ni Eloah, ni Mwenyezi na
ndiye mwanzo wa uumbaji pamojja na
uumbaji wake. Anaanikiza uweza huu kwa Masihi kwa ujio wake (Ufunuo
22:13). Jambo hili limeainishwa pia kwenye jarida la Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na. 229)).
Ushirikishaji wa Eloah kwa Elohim kama
muundo wa uwingi pia unaonekana kiashirio kwenye matumizi ya jina
Yahova (Kamusi ya Strongs Hebrew Dictionary (SHD) 3068)
na Yahovih (SHD 3069). Kuna viumbe wengi wanaojulikana na kuitwa jina
hili la Yahovah, (pia wanaitwa Yehova au Yahweh kwa wengine) kwenye Agano
la Kale. Yahovah anajulikana kama Mungu wa kitaifa wa Israeli na
anajulikana kama Adonai na Wayahudi wanapolisoma jina
lake. Yehovih anajulikana kama ni Mungu na anaitwa elohim na
Wayahudi wanapokuwa wakiyasoma maandiko. Viumbe wawili wanahusishwa. Na hii
ndiyo maana Yahovah alibadilishwa kuwa Adonai mara 134 kwenye Agano
la Kale na baraza la Sopherim. Yahovah ni jina la kicheo lililotolewa
linaloainika kwa viumbe wengi kama ilivyokuwa kwa suala wakati Yahovah watatu
walipojitokeza na kunena na Ibrahimu kabla ya kuangamizwa kwa Sodoma na wawili
kati yao walikwenda kwa Lutu huko Sodoma. Kulikuwa na Yahovah wa nne
Mbinguni waliounyeshea moto mji wa Sodom (soma Mwanzo 19:24). Maandiko haya
yalibadilishwa na baraza la Sopherim (kwa mujibu wa The
Companion Bible, Appendix 32; na soma pia jarida la Mkururu wa Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara 1: Asili ya
Mungu (Na. 003)).
Swali lote la mwanzo wa nyakati limeainishwa kwenye
jarida la Serikali ya Mungu (Na. 174).
Kuna wakati ambapo Roho alikuja kuwa na uhusiano na siyo kwa kushirikishwa
kwenye mamlaka ya kimungu kama mbadala wa Mungu. Mungu alikuwepo kuwa ni wa
milele. Ni yeye tu ndiye hafi wala kupatwa madhara (1Timotheo 6:16). Mungu ni mfalme na Bwana wa nyakati zote (1Timotheo
1:17; sawa na yasemavyo maandiko ya Kiyunani ya Tobiti 13:6,10) na Mungu wa nyakati zote (theos tõn aiõniõn,
sawa na Ecclus. 36:17; Isaya 9:6; Yeremia 10:10). Harakati za uumbaji wa Mungu
ulianzisha udugu wa Roho kuweka nyakati. Mungu alianikiza uweza wa kuwa
asiyeweza kufa wala kupata madhara kwa wana wa Mungu tangu kuumbwa kwao. Kwa
uumbaji wa mwenendo huru au wa kujitegemea kwa Roho, kama mwingiliano wenye
weledi mkubwa wa Mungu, zama zikaanza.
Mwanzo
Mungu alianza kuumba. Tendo la kwanza la uumbaji, kwa
uzao lilikuwa ni kumhuluku Mwanae aliyemfanya elohim. Huu ulikuwa ni uumbaji wa
kiroho. Hawa wana wa Mungu walikuwa ni wengi. Roho Mtakatifu alikuwa ni uweza
au kiini chimbuko takatifu na nguvu iliyowaunganisha elohim hawa wawili na
ambaye aliwawezesha kuwa wamoja na Mungu (soma majarida ya Roho Mtakatifu (Na. 117); Uzima wa Milele (Na. 133); Kufanyika Sawa na Baba (Na. 081); Jinsia ya Roho Mtakatifu (Na. 155); Manabii Wajumbe wa Mungu (Na. 184); Mungu Mwokozi Yetu (Na. 198)).
Nyakati zilianza kwa kuumbwa kwa Jeshi la Malaika (soma pia kitabu cha
Augustine cha Mji wa Mungu; na jarida la Mji wa Mungu (Na. 180)).
Baraza la Hawa Elohim Kama Wana wa Mungu
Wana wa Mungu walihisishwa kwenye muundo huu. Waliongozwa
na Baraza, ambalo limeonekana kwenye Kitabu cha Ufunuo. Linajumuissha viumbe
ishirini na tisa wanaokizunguka kiti kitukufu cha Mungu. Kuna wazee ishirini na
walio chini ya kuhani mkuu. Kuna pia maserafi (wanaoitwa viumbe wenye uhai
kutokana na jinsi vichwa vhao vinavyoonekana). Shetani alikuwa ndiye yule Kerubi
afunikaye kwenye Kiti cha Enzi cha Mungu (Ezekieli 28:14).
Baraza hili linaitwa Baraza la Elohim au Baraza la
Mungu na Viumbe wengine wateule wa Mbinguni. Uumbaji halisi ulifanywa na
elohim.
Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo
Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Dunia ilikuwa bado ingali tupu haina kitu. Giza lilitanda
juu ya uso wa vilindi na Roho wa Mungu alituama juu ya uso wa vilindi vya maji
(Mwanzo 1:2).
Huyu elohim ndiye aliyemuumba mwanadamu kwa
sura na mfano wa elohim baada ya kufanana na wao.
Mwanzo 1:26-27 Mungu akasema, Na
tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu
akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba.
Hapa elohim anapanga mkakati wa kumuumba mwanadamu (adamu pasipo
kutumia zana wala kiambata chochote; akafanyika kuwa binadamu) kwa sura na
mfano wake. Aya ya 27 ndipo inapunguza idadi kwa umoja vile aliyeumba. Mtu aliyeumbwa
hapa ni adamu kwa
kiambata, na ndiye Adamu. Kwahiyo kuna mambo mawili kwenye uumbaji huu.
Kwahiyo uumbaji
imefanywa kotekote, yaani mbinguni na duniani (Mwanzo 2:1). Tunajua kutokana na
Kumbukumbu la Torati 32:8-9, kwamba Mungu Aliye Juu Sana aliyaanzisha mataifa
sawasawa na Wana wa Mungu (bene Eliym; DSS) au malaika wa Mungu (‘agellon theou;
LXX). Mandiko ya Masoretic yalibadilishwa, wakati fulani baada ya
Kristo, kuyasoma kwa mujibu wa idadi ya
Wana wa Israeli.
Kumbukumbu la Torati 32:8-9 Yeye Aliye Juu alipowapa
mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya
hesabu ya wana wa Israeli. 9 Maana, sehemu ya Bwana ni watu
wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.
Tafsiri ya RSV inakubaliana na andiko sahihi kwenye tafsiri
yake. Kulikuwa na Wana wengi wa Mungu (soma pia jarida la Uwepo wa Kristo Kipindi cha Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi
Duniani (Na. 243)).
Nyota za Mungu
Mungu Aliye Juu Sana anajulikana kama Baba na muumbaji,
kutokana na Kumbukumbu la Torati 32:6.
Kumbukumbu la Torati 32:6-7 Je! Mnamlipa Bwana hivi,
Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua?
Amekufanya, na kukuweka imara. 7 Kumbuka siku za kale,
Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonyesha; Wazee
wako, nao watakuambia.
Kwahiyo, Mungu Aliye Juu Sana ni Baba na Wana wa Mungu ni
wazee. Yahovah aliye kwenye andiko hili ni mshirika wa Mungu wa Israeli.
Kwa hiyo, jina Yahova ni mamlaka yaliyotokana na Mungu Aliye Juu Sana ambaye ni
Baba. Aliwafanya elohim na kuwaweka kwenye mataifa sawasawa na idadi yao,
ambayo kwa kweli ni sabini. Kuna Mabaraza yote mawili ya Wazee au Elohim,
ambayo ni la ndani na la nje. Yahova amewekwa aketi kwenye Baraza hilo. Alitiwa
mafuta kuwa Mungu wa Israeli ili kuanzisha mpango wa wokovu wa Mungu, ambao
ulikuwa ni wa muhimu kutoka kwenye Bustani ya Edeni na uasi wa Malaika, wakati
Shetani alipowekwa kwenye Bustani ya Edeni awe kama Kerubi au Nyota ya Asubuhi au Nyota ya Siku au ya
Mchana (soma jarida la Fundisho la Chanzo au
Chimbuko la Dhambi Sehemu ya I Bustani ya Edeni (Na. 246)).
Cheo cha Nyota ya Asubuhi kilikuwa cha wengi tangu
uumbaji na kimeainika hadi kwa Kristo na kwa wateule.
Ayubu 38:4-7 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi
ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. 5 Ni nani
aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? 6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani
aliyeliweka jiwe lake la pembeni, 7 Hapo nyota za
asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
Kulitakiwa kuwe na nyota inayotoka kwa Yakobo kwa mujibu
wa Hesabu 24:17. Hii ilitakiwa kuchukua nafasi ya ile nyota iliyoanguka kutoka
mbinguni (Ufunuo 8:10). Hii inamwashiria Kristo aliyechukua mahali pa Shetani
kama Nyota ya Asubuhi (soma pia jarida la Lusifa: Mpeleka Nuru na Nyota ya Asubuhi (Na. 223); Kusudi la Uumbaji na Dhabihu ya Kristo (Na. 160); Stadi wa Uumbaji wa Mungu Kama Alfa na Omega (Na. 229)).
Nyota ya Siku au Nyota ya Asubuhi inapambazuka mioyoni
mwetu (2Petro 1:19). Tumepewa huyu Nyota ya Asubuhi kwa kupitia Kristo (Ufunuo
2:28; 22:16). Wote ni wadogo na wasaidizi kwa Mungu Aliye Juu Sana.
Mwana ambaye ndiye alikuwa Elohim wa Israeli
Israeli waliuelewa uhusiano huu wa aliye mkubwa na bora
na aliye mdogo na elohim msaidizi. Iliaminika na kujulikana kuwa Baba ndiye
aliye Bora na Mkuu zaidi au ni Mungu Aliye Juu Sana. Alikuwa pekee kama Eloah,
El wa El. Mwana wa Mungu aliyetiwa mafuta awe kama
Yahovah au Elohi wa Israeli alikuwa mdogo.
Zaburi 45:6-7 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni
cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 7 Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu
wako, amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.
Anayenenwa hapa ni Elohim wa Israeli tunayemjua
leo kama Yesu Kristo.
Waebrania 1:8-9 Lakini kwa habari za
Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya
ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki,
umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe
kupita wenzio.
Kipindi chote cha hadi kuzaliwa kweke Yesu Kristo hapa
Duniani, cheo chake kilikuwa ni kama mmoja wa hawa elohim tu, na alipokuwa
anatenda jambo lolote, nao walionekana kuwa walikuwa wakifanya vivyohivyo.
Aliinuliwa juu zaidi kuliko wenzake wengie wote kwa kufufuka kwake kutoka
mautini akiwa kama Mwana wa Mungu mwenye uweza kwa kupitia Roho Mtakatifu.
Warumi 1:4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa
Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo
Bwana wetu;
Uwingi huu wa hawa elohim unaonekana kwenye fafanuzi za
Wafilisti.
1Samweli 4:8 Ole wetu! Ni nani
atakayetuokoa na mkono wa miungu hawa walio hodari? Hawa ndio miungu
waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani.
M8iungu hawa
wenye nguvu wanaotajwa hapa wanaonekana moja kwa moja kuwa ni elohim wenyewe.
Kwa hiyo, Yahovah aliwaambia hawa elohim. Mwana wa Mungu kwenye
jeshi la Israeli alitenda kazi kwenye mamlaka na sambamba na Baraza ambalo
walikuwa ni washirika wake (metoxous Zaburi 45:6-7 LXX; Waebrania
1:8-9). Mataifa yalielewa pia uwingi huu wa hawa elohim.
1Wafalme 20:10 Ndipo Ben-hadadi akatuma
kwake, akasema, Miungu wanifanyie hivi na kuzidi, yakiwa mavumbi ya Samaria
yatatosha makonzi ya watu wote walio miguuni pangu.
Miungu inayotajwa hapa
ni elohim. Kwa hiyo Ben-hadad alimjua huyu elohim.
Yahovah wa Israeli anatoa hukumu katikati ya elohim.
Zaburi 82:1 Mungu asimama katika
kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.
Hapa, elohim amechukua mahala pake kati ya miungu au
El. Katikati ya hawa elohim anatoa hukumu. Andiko linaendelea kwa
kuainikiza Uwana huu kwa Jeshi lote la malaika. Kama tujiavyo, huyu ilieleweka
kama mteule na Irenaeus (soma jarida la Teolojia ya Mwanzoni ya Uungu (Na. 127)).
Zaburi 82:6 Mimi nimesema, Ndinyi
miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
Miongoni mwa elohim ilichukuliwa kuwa hakuna aliye
kama Yahovah (Yehova) (aliyetafsiriwa hapa kama Bwana).
Zaburi 86:8 Katikati ya miungu hakuna
kama Wewe, Bwana, Wala matendo mfano wa matendo yako.
Yoshua au Yesu Kristo wa Agano Jipya
Ni muhimu sana kwamba tunajua hiyo inatokea kwenye Agano
Jipya na mahali jina Yesu linapotokea na kile ambacho matumizi yake
yanakusudiwa kumaanisha.
Yesu halikuwa jina la Yesu Kristo, yaani Masihi. Jina
lake lilikuwa ni Yoshua au Joshua
kwa matumizi ya Kiingereza, ambalo siyo kwa J ya mkato, bali ni matamko ya J
laini. Jina la Joshua limekuwa hivyo mara kwa mara kwenye matumizi ya
Kiingereza kwa kipindi cha maelfu ya miaka. Linaonekana kidodoso kwenye Agano
la Kale na kwenye sura kadhaa za Agano Jipya. Kiyunani cha Agano Jipya
kinatumia miundo ambayo ilikutikana kwenye tafsiri ya Septuagint ya Maandiko
Matakatifu ya Kiebrania, ambayo yalitafsiriwa huko Alexandria yapata miaka
takriban mia tatu kabla ya Kristo.
Maandiko Matakatifu ya Septuagint yalikuwa na malengo
yaliyofikiwa yenye maana sana. Yana kiwango mwanana cha aina ya Kiyunani chenye
maneno ya Kiebrania. Ièsous ni jina la Kiyunani la kwenye tafsiri ya
Septuagint lenye maana ya neno Yoshua au Joshua kwenye Maandiko
Matakatifu ya Agano la Kale. Septuagint ilikuwa ni Biblia ya Agano Jipya. Nukuu
nyingi zilizonukuliwa kwenye Agano Jipya zinatokana na tafsiri hii ya
Septuagint (LXX). Septuagint ilikubalika kuwa ni Maandiko Matakatifu wakati wa
Kristo. Ililaumiwa na kuonewa mashaka na Mafarisayo kipindi cha baada tu ya
kuangamizwa kwa Hekalu, na kutotumiwa au kuchukiwa na marabi, baraza
lililofanyika hatimaye kuwa ni warithi jopo la Kifarisayo, kipindi cha baadae yapata
kama kwenye karne ya pili hivi.
Kwa hiyo, wakati wa Kristo kulikuwa na mabishano
kuhusiana na Septuagint kuwa kama ni Maandiko Matakatifu ama la. Kwa kweli
inaweka misingi ya Agano Jipya. Maneno ya Kiyunani kwenye Septuagint yalitumika
kwa majina ya tabia na mwenendo wa Kanisa la Agano Jipya na kwamba Kiyunani
hatimaye kilitafsiriwa kwa Kiingereza kipindi cha baadae sana. Karne nyingi
zilizofuatia ziliendeleza kuandikwa kwa tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza
za Agano Jipya.
Sasa tatizo likuwa kwamba, neno Yoshua lilitafsiriwa
kutokana na neno la Kiyunani ambalo liliandikwa Joshua, ambalo linajitokeza
mara nyingi kwenye Agano Jipya, na linahusiana na idadi kadhaa ya watu
mbalimbali na limetafsiriwa kwa namna nyingi mbalimbali. Kwa mfano, kwenye tafsiri
ya KJV, Waebrania 4:8, neno lililotumiwa la Joshua lilitafsiriwa kama Jesus
(Yesu) mara nyingi sana, na kufanya kwamba lionekane neno Yoshua na kwenye
Agano Jipya lote lisomeke Yesu kutokana na neno la Kiyunani
la Ièsous kuhusu Yoshua. Lakini Waebrania 4:8 inamtaja Yoshua mwana
wa Nuni na ndivyo linavyojulikana na Biblia nyingine zote zinapomtaja Yoshua
mwana wa Nuni. Bullinger kwenye uandishi wake wa Companion Bible
anakubaliana kwamba Waebrania 4:8 haikusudii kumtaja Yesu, kwa maana ya kuwa ni
Kristo, bali inakusudia kumtaja Yoshua mwana wa Nuni.
Yoshua mwingine aliyeitwa Yusto kwenye Wakolosai anaitwa
pia kuwa ni Yesu aitwaye Yusto (Wakolosai 4:11). Kuna mionekano mingine na
kutajwa kwa Kristo kwenye mistari ya uzao wa Yesu. Kwenye Luka 3:29 tunasoma
kwamba Yoshua huyu alikuwa ni mwana wa Eliezeri. Sasa neon hili lililotafsirwa
Yoshua ni neno la Kiyunani la Yoshua anayeitwa Yesu. Hakuna andiko
linalomaanisha kikamilifu sana kwa mba Yoshua mwana wa Eliezeri na baba wa
Eri ni kwa hakika anaitwa Yesu. Hii ni kwa sababu tu kwamba ni namna ya
kuandika kwa Kiyunani kwa jina Yoshua kwa kutumia kanuni iliyoanzishwa kwenye
Septuagint. Tafsiri ya KJV inaubadilisha au kuugeuza ukweli huu kwa kumtaja
Yoshua hapa kama Yose. Kanuni hii ya Kiyunani inayoandika Yoshua inafuatiwa
kwenye Waebrania 4:8 na mahali penginepo. Kuna mtu mwingine ambako limetumika
neno Ièsous na limetafsiriwa kama kitu fulani tena. Kina Yoshua wengi
mbalimbali wameandikwa kwenye maandiko wakiitwa
Jahoshua (au Yahoshua) na pia Yeshua, Yeshuah, Hosea, Hoshea, Osea lakini
tofauti zilifanywa pia kwenye Kiebrania.
Matumizi yenye kulinganishwa kwenye nakala ya Septuagint
yanaonekana kutoka kwenye jaribio la kila mfano wa neno
Yahoshua au Yahshua kwenye Kiebrania cha Agano la Kale na ambapo
imechukuliwa hivyohivyo kwenye lugha ya Kiingereza likijulikana kama Joshua.
Kwenye kila mfano, neno Yoshua limechukuliwa kama Yesu au Ièsous kwenye
Kiyunani. Neno Yesu ni tafsiri ya Kiyunani na siyo sahihi kulichukulia kama
lilivyo kama jina lilivyo kwenye lugha ya Kiingereza kwa maana hiyohiyo. Ukweli
wa mambo ni kwamba neno Ièsous ni la Kiyunani linalomaanisha Yoshua
na unapotafsiri Kiyunani kwenda kwenye lugha ya Kiingereza kwa kuyatumia
Maandiko Matakatifu ya Kiebrania, ndipo Septuagint inaunda kanuni. Kanuni ya
majina ni kwamba imetumika kwenye kwenye maana iliyokubalika ya Kiingereza,
ambapo Maandiko ya Kiebrania yametafsiriwa kwenye lugha ya Kiingereza.
Kwa hiyo wakati neno Ièsous linaonekana kwenye
Agano Jipya kwa kanuni na uandishi wa Septuagint, linamaanisha Yoshua, ambalo
limekuwa ni kigezo mizania cha jina kwa karne kadhaa sasa. Wanazuoni waamini
Utatu walipokuwa wakitafsiri toleo la KJV kwenye lugha ya Kiingereza,
walijaribiwa kuweka tofauti kati ya Agano Jipya na Agano la Kale na kuondoa
uhalisia na watu kwenye Agano Jipya kutoka kwenye Agano la Kale ili kwamba
muendelezo wa Agano Jipya na Agano la Kale ubadilike. Hivyo mgawanyiko
ulijitokeza kati ya kanuni kama imetokana na Biblia. Sheria au Torati ya Mungu
kwenye Agano la Kale ilifanywa kuwa ni tofauti na kile kilichokuwa kikitokea
kwenye tukio la Mashihi (Tukio la Kimasihi la Yoshua, Masihi kwenye Agano
Jipya). Hivyo walimuita Yesu Kristo ambalo maana yake ni Yesu Mtiwa Mafuta.
Yoshua Masihi maana yake ni Yoshua Mtiwa Mafuta. Kwa hiyo neno hili kama
linavyoonekana kumhusu Mtiwa Mafuta linamlenga kwenye lugha ya Kiingereza
kwenye Agano la Kale Masihi na walikuwepo wengine wengi zaidi ya Masihi mmoja.
Kwa hiyo Yoshua ni jina sahihi a
huyu Ièsous kwa Kiyunani, ambapo bila shaka kwenye muundo wa kifonetikali,
unaoweza kumtaja ukimaanisha kwa muundo wa Agano Jipya na bila shaka unapokuwa
unasoma Agano la Kale bado utakuwa unasoma (au unaweza kusoka) Yoshua kama
ni Ièsous pia kwa kumaanisha, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwenye tafsiri
ya LXX. Hatuna tahshishi na kuongea Kiyunani. Tunahusika na kusema Kiingereza,
kwenye tafsiri za Kiingereza tukirejea nyuma kwenye tabia na kanuni za Biblia
ili kwamba kuna muundo sahihi, uliowazi na endelevu unaoendelezwa, na Agano
Jipya halijajitenga na Agano la Kale.
Kuna Biblia moja tu, inayojitosheleza kikamilifu sana kwa
mamlaka na inayoshabihiana pasi kupingana. Ni muhimu sana kujua kwamba wakati
Biblia inapotafsiriwa kwenda kwenye lugha zingine, kwamba mambo muhimu yaliyo
kwenye Agano Jipya pamoja na majina hayo yatafsiriwe kwa namna iliyo sahihi
zaidi. Na kwamba yabebe majina ambayo tabia na uhalisia ambao wahusika
walikuwanayo kwenye Agano Jipya pamoja na majina hayo yawe yametafsriwa
kiusahihi zaidi. Ndipo hatimaye wanayasikia majina kwamba sifa hizo za walengwa
zilikuwemo kwenye Agano la Kale kwenye lugha ambayo imetafsiriwa kwayo; hata
kama ni Kirusi, Kiukraini, Kifaransa, Kijerumani, Kidachi, au kwa lugha
nyingine yoyote ile. Na kwa kweli ni makosa na siyo sahihi kufanya tofauti hizi
na hailengi kusudio lolote la msingi, zaidi
ya lile la kuipa mashiko na kuisaidia imani potofu ya Utatu na mafundisho
potofu ya teolojia ya ki Antinomia ambayo yalikuwa ni kisababishi kikubwa cha
tafsiri hizi za kijanja kwa mahala pa kwanza. Ni muhimu kwamba tunafanya
marejesho ya kusudio halisi na muundo wa Maandiko Matakatifu.
Yoshua lilikuwa jina la Kristo Masihi, kwa kuwa linamaana
ya Wokovu wa Mungu. Yoshua mwana wa Nuni aliitwa Wokovu wa Mungu, Mwana wa
uvumilivu, ikimaanisha kwamba wokovu huja kwa uvumilivu. Maana ya jina la
Masihi yalikuwa ni Wokovu huja kama Mwana wa Mungu. Wokovu wa Mungu unatoka kwa
Mungu. Na hii ndiyo maana iliyopelekea Masihi aitwe Yahoshua ua
Joshua kwa Kiingereza na sababu jina Yesu aliudhihirisha ukweli huo.
Kwa mfano unaposhughulikia suala la mama wa Masihi,
tunaona kwamba jina lake lilikuwa ni Mariam na jina lake ni
Mariam wakati wote kwenye Agano Jipya lote. Jina la mdogo wake lilikuwa ni
Maria. Kwa hiyo jina Mary siyo jina linalojitokeza kabisa kwenye Agano Jipya.
Ni upotofu tu uliofanywa na Waanglikana walioweka jina hili la Maria na huyo
Maria hakuwa mama wa Kristo kabisa. Kwenye kila mfano isipokuwa mmoja tu,
ambapo kuna tofauti fupi sana kumetumika Mariamu ambalo ndilo jina la mama yake
na Maria ni jina la shangazi yake. Baba yake alikuwa Yusufu. Tunajua hivyo.
Hawakupata shida kuhusu yusufu, lakini wanawaelezea ndugu wa Kristo, badala ya
kujataja majina ya kawaida kwa Kiingereza kuhusu hawa ndugu zake, wanawaficha
na kuwageuzia mbali.
Mambo haya yapaswa yajulikane. Tutayaelezea kwa kina kwenye
utangulizi wa kitabu cha fafanuzi kuhusu Biblia na hususan kwenye Agano Jipya
wakati tutakapoyachambua majina na kuyaelezea kwa ufafanuzi wa kina matumizi
yake. Haionyeshi maana nzuri kuendelea kufanya nadharia upotoe uliopo kwenye
uanzishwaji wa kanisa la mrengo wa
Kitrinitarian la Kiingereza, kwamba limefanya uharibufu mkubwa zaidi
kwenye uelewa wa Teolojia ya Biblia na Sheria za Mungu, kuliko taasisi nyingine
yoyote ile kwenye ulimwengu wa watu wanaoongea lugha ya Kiingereza. Kristo
angewakataa na atawakataa kabisa na kuwaona kuwa ni wazushi wa kimafundisho na
wapotofu. Hii haimaanishi kwamba tuufuate upotofu wao. Ukweli wa Biblia yapaswa
urejeshwe kiuwazi sana na kikamilifu sana.
Mungu wa Miungu
Bwana ndiye El Mkuu na ni Mfalme juu ya elohim wote.
Zaburi 95:3 Kwa kuwa Bwana ni Mungu
mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
Elohim wa mataifa anachukuliwa kuwa si kitu
(ametafsiriwa kama kinyago au sanamu).
Zaburi 96:4-5 Kwa kuwa Bwana ni mkuu
mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. 5 Maana
miungu yote ya watu si kitu, Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.
Bwana anayetajwa
hapa ni Yahovah aliyeinuliwa juu kuliko elohim wote. Jambo hili linaibua mambo
fulani ya muhimu sana kuhusu Yahovah (Jehovah) ni kama jina tuliloliona hapo juu.
Zaburi 97:7-9 Na waaibishwe wote
waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni
Yeye. 8 Sayuni imesikia na kufurahi, Binti za Yuda
walishangilia, Kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana. 9 Maana
Wewe, Bwana, ndiwe Uliye juu, Juu sana kuliko nchi yote; Umetukuka sana juu ya
miungu yote.
Hapa Yahovah anatajwa kama Mungu Aliyejuu sana.
Hivyo tunaongelea vitu viwili tofauti, Yahovah wa Israeli
na Yahovah Alye Juu sana (au Jehovah) Aliye Juu sana kulik
elohim wengine wote.
Kuhani Mkuu na Mungu wa miungu
Zaburi 135:5 Maana najua mimi ya kuwa
Bwana ni mkuu, Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.
Hapa Adonim au Bwana wetu ni yeye aliye juu ya
elohim wote. Kwa hiyo mtangulizi aliyepo hapa ameinika kuwa Elohim wa
Israeli. Kwa hiyo ameonekana na kufanywa kuwa ni Kuhani Mkuu wa Elohim.
Hata hivyo yeye siyo Elohim wa Elohim. Hii imeachwa kwa
Eloah au Yahovah Aliye Juu Sana.
Zaburi 136:2 Mshukuruni Mungu wa
miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Yeye peke yake ndiye adonim wa adonim au
ni Bwana wa Mabwana. Aliunda uwakilishi na hivyo ni uwingi wa andiko lililo
kwenye Yeremia 10:10-11.
Yeremia 10:10-11 Bali Bwana
ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za
ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake. 11 Mtawaambia
hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo
itatoweka chini ya mbingu.
Kuna Mungu mmoja tu wa kweli kama tunavyoona. Yeye
ni Mungu aliyehai na ni mfalme wa milele. Hawa elohim wana majukumu mbalimbali
kwenye uumbaji. Mungu mmoja, wapekee na wa kweli aliiumba dunia kwa uweza na
hekima yake.
Yeremia 10:12-13 Ameiumba
dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu
wake amezitandika mbingu.13 Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji
mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme,
Huutoa upepo katika hazina zake.
Tendo hili la uumbaji lilifanywa kwa utadi mkubwa na
Mungu. Majukumu mengine ya uumbaji yalibebwa na Masihi, mzaliwa wa kwanza wa
uumbaji. Hata hivyo, jukumu na jambo moja linahitaji ufafanuzi.
Waefeso 3:9 na kuwaangaza watu wote
wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika
katika Mungu aliyeviumba vitu vyote;
Maneno ya dia ‘Iesou Christou au kwa
Yesu Kristo hayako sahihi. Maneno haya yapo kwenye tafsiri ya
Receptus na kisha kwenye KJV lakini hayajitokezi wala kuonekana kwenye
maandiko ya zmani. Hayaonekani kwenye tafsiri za kisasa za Biblia. Tafsiri ya
RSV kiusahihi zaidi inaandika andiko hili kama h9ivi:
Waefeso 3:9 na kuwaangaza watu wote
wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika
katika Mungu aliyeviumba vitu vyote;
Wakolosai 1:15-20 naye ni mfano wa Mungu
asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Kwa
kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,
vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi,
au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote
hushikana katika yeye. 18 Naye ndiye kichwa
cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu,
ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19 Kwa
kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; 20 na
kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu
ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo
mbinguni.
Tazama jinsi inavyosema yeye ni mwanzo (yani
Khristo).
Muundo wa kiuongozi wa utaratibu wa kidini haupaswi
ukanganywe na viumbe wa elohim wenyewe. Huyu wa kale anayetajwa hapa kwenye Wakolosai amekusudiwa kwenye
kuyashinda malumbano yanayohusu uumbaji wa ulimwengu kwa kupitia suala ambalo
lenyewe tu lilichukuliwa kuwa ni wakale (soma
kwenye majarida ya Roho Mtakatifu (Na. 117); na Mwendelezo wa Mtindo wa Kiplatoniki Mamboleo (Na. 017)).
Ilikuwa ni kizazi cha Kristo na wana wa Mungu ambacho
kilikuwa ni cha mwanzoni mwa uumbaji wa Mungu. Mwanzo huo wa uumbaji wa Mungu
ndiyo unaomaanishwa kwenye Ufunuo 3:14.
Katika Kristo utimilifu wote wa Mungu ulipendezwa uwepo.
Kwa hiyo, Kristo ni kifaa au chombo cha Mungu kama mwanzo wa uumbaji wake.
Alikuwa ni mzaliwa wa kwanza katika wafu ili kwamba kwenye vitu vyote aweze
kuwa kwenye mahali pa kwanza. Hata hivyo, vitu vyote vina Baba mmoja na chanzo
kimoja na muumbaji mmoja ambaye kwa yeye tu peke yake ndiye Mungu mmoja, wapekee
na wa kweli.
Malaki 2:10 Je! Sisi sote hatuna Baba
mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda
ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?
Huyu Baba ndiye Bwana wa Majeshi (Malaki 1:6). Anaanikiza
nafasi ya Ubaba kwa elohim kwa kuwapa mamlaka. Isaya 9:6 inaendelea kuanikiza
Ubaba huu kwa Masihi. Kuna aina nyingi za Ubaba au mababa (Patria)
mbinguni na hapa duniani na wamejulikana na kuitwa Mababa (Waefeso 3:14).
Waefeso 3:14-15 Kwa hiyo nampigia Baba
magoti, 15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni
na wa duniani unaitwa,
Dhana ya Kuzaliwa Hapa Duniani ki Mabadiliko ya Zama Moja
Hadi Nyingine Kimaumbile
Waebrania 1:6 inamtaja kiumbe aliye mzaliwa wa kwanza
aliyetumwa na kuletwa duniani. Kiumbe huyu, mzaliwa wa kwanza (prõtotokos)
wa kila kiumbe anayetajwa kwenye Wakolosai 1:15, ametambuliwa kama Mwana. Mwana
ndiye pia prõtotokos wa Mariamu (au Maria) (Mathayo
1:25; Luka 2:7). Huyu Mwana alikuwa pia ni prõtotokos miongoni
mwa ndugu wengi. Hivyo basi, jina hili linamaanisha wa kwanza kwenye mkururu
ambao unajulikana kama anayestahili.
Waamini utatu wengine wanafikia hata kudai kwamba
Mariamu (Maria) hakuwa hata na watoto wengine. Huu ni uwongo. Kristo
alikuwa na ndugu wengine wengi, wakike na wa kiume (Mathayo 13:55-56); (sawa na
lisemavyo jarida la Bikira Mariamu na Familia ya Yesu
Kristo (Na. 232)). Majina ya hawa ndugu wa
kiume wa Kristo yalikuwa ni Yakobo, aliyeitwa James na Wapagani Yusufu
aliyeitwa jina la baba yake, Yuda aliyeitwa jina la kabila lake; na Simeon.
Majina ya dada zake yalikuwepo lakini hayakuandikwa, lakini majina haya yako
wazi na yanajulikana sana na yanatofautiana na yameandikwa kwenye Kiingereza
kutokana na Agano la Kale. Kuna sababu ya muhimu sana na ya wazi kwanini
yalibadilishwa. Ilikuwa ni kukusudia kukanusha ukweli wa kwamba Kristo alikuwa
na ndugu wengine wa kike na wakiume na ili kumtukuza zaidi Mariamu ili astahili
kuongekana kuwa ni mungumke mlengwa wa ibada za Easter na imani hii. Kupinga au
kukataa kwamba Mariamu (Maria) hakuwa na watoto wengine ni makosa makubwa
wakati inaonekana wazi kwamba kuna mtoto anayeitwa Yusufu mwanawake Mariamu,
mmoja wa ndugu wa Kristo, na jina la baba yake aliitwa Yusufu. Ni ukweli ulio
wazi sana kwamba alikuwa anaitwa jina la baba yake. Haya ni majina ya kifamilia
ambayo unatarajia kuyaona kwenye familia ya Kristo.
Masihi hapa ni mzaliwa wa kwanza pia wa wafu. Kwa hiyo
yeye ni mwanzo akiwa kama kichwa cha mwili na ushirika huu. Kwa muktadha huohuo
alikuwa pia mwanzo wa uumbaji wa Mungu (Ufunuo 3:14). Muundo wote mzima
uliwekwa na Mungu kwa kuruhusiwa. Kwa hiyo alikuja ili awepo ili aweze
kukamilisha mpango wa Mungu kama ilivyofanyika kwa viumbe wengine wote.
Kutanglia mbele kwa Masihi kunapatikana kutokana na mpango wa Mungu na kwa amri
ya Mungu (soma jarida la Stadi wa Uumbaji wa Mungu
Kama Alfa na Omega (Na. 229)).
Tunajua kutokana na Tunajua kutokana na Yohana 17:3 na
1Yohana 5:20 kwamba Mungu huyu Mmoja, Wapekee na wa Kweli ni Baba na kwamba
Yesu Kristo ndiye mwana wake.
Yohana 17:3 Na uzima wa milele ndio
huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
1Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana
wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,
nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu
Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Mungu huyu mmoja, wa Pekee na wa Kweli ndiye uzima wa
milele. Tumepewa uelewa huu na Mwana wa Mungu ili kwamba tuweze kumjua yeye
aliye wa kweli na kwamba tuweze kuwa ndani yake yeye aliye wa kweli na ndani ya
mwanawake Yesu Kristo au Yoshua Masihi. Mungu huyu mmoja ana uzima wa milele.
Ni yeye tu ndiye hafi wala kupatwa na madhara yoyote.
1Timotheo 6:13-16 Nakuagiza mbele za Mungu
anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo
mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14 kwamba uilinde
amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu
Kristo; 15 ambako yeye kwa majira yake
atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme,
Bwana wa mabwana; 16 ambaye yeye peke yake hapatikani
na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu
aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
Ilimpasa Masihi auachiliembali uzima wa milele aliokuwa
amepewa na Baba na akakubali kuwa na mwili wa kibinadamu. Aliachilia mbali
uzima wake kwa kuamriwa na Baba na akauchukua tena kwa amri ya Baba (Yohana
10:17-18).
Yohana 10:17-18 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu
nautoa uhai wangu ili niutwae tena. 18 Hakuna mtu
aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na
uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.
Hivyo, ni Mungu huyu ndiye anayetoa uzima kwenye vitu vyote.
Kurudi Mara ya Pili
Kurudi na kuonekana kwa Mwana wa Mungu kumefanywa
kudhihirike wazi kwa wakati sahihi na yeye aliye Mkuu wa kipekee ambaye ni
Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana nay eye pekeyake ndiye hafi wala kupatwa
na madhara (soma jarida Uzima wa Milele (Na. 133) na Kwenye Hali ya Kutokufa wala Kudhurika (Na. 165)).
Amemkabidhi Mwana mambo haya ili kuanzisha Ufalme wa Mungu kama tunavyoona
kwenye Ufunuo 17:14 na 19:16. Majina haya yameandikwa kwenye kanzu au vazi na
kwenye paja la Masihi.
Ufunuo 19:11-16 Kisha nikaziona mbingu
zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na
Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na
macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi;
naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina
lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo
mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe,
safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige
mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo
la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye
ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA
WA MABWANA.
Mungu hufanya kazu kwa kupitia Mwana wa Mungu kama
alivyomfanya kuwa kuhani mkuu
Neno la Mungu ni Mwana wa Mungu. Huyu Mwana
alikuwa pamoja na Mungu hapo mwanzoni. Huyu ndiye alikuwa (au aliendelea) na
Mungu (ton theon) na huyu alikuwa ni theos au elohim.
Tunajua kuwa huyu elohim ni mdogo (soma Zaburi 45:6-7; Waebrania 1:8-9). Paulo
anakubali kwamba hakuna Mungu mwingine (theos) ila ni mmoja tu; akini
kulikuwa na miunguu wengi (theoi) (theoi polloi) na mabwana
wengine pia (kurioi) mbinguni, lakini kulikuwa na Mungu mmoja tu aliye
Baba na Bwana mmoja Yesu Kristo (1Wakorintho 8:5-6; soma Kamusi ya Marshall’s
Interlinear). Kazi na shughuli zote zitakuwa zimewekwa chini ya hawa na
utaratibu na huduma zote za Hekalu zitarejeshwa upya, kwa kweli; kote kuwili,
mbinguni na duniani.
Mungu alichagua kutenda kwa uwakilishi kwa Mtakatifu wake
ambaye ndiye aliyemtia mafuta mfalme wa Israeli kama tunavyojionea kwenye
Zaburi 89:18-20.
Zaburi 89:18-20 Maana ngao
yetu ina Bwana, Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli. 19 Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa
njozi, Ukasema, nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa
miongoni mwa watu. 20 Nimemwona
Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
Tafsiri ya RSV inaonekana kuligeuza au kulipotosha andiko
hili huenda ni kutokana na mwelekeo wake (soma kamusi ya Green’s Interlinear
ili kujipatia maana na maandiko zaidi).
Utaratibu wa kimbinguni uliwekwa kwa kufananishwa na ule
wa Hekalu la Duniani la Israeli kutokana na maskani, ambalo limefananishwe na
Hekalu la Sulemani.
Waebrania 8:5 watumikiao mfano na kivuli cha
mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya
ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa
katika mlima.
Tunaona pia kwamba kulikuwa na makerubi watiwa mafuta
wawili wafunikao, au Makerubi wa kwenye maskani, (Kutoka 25:18-22) waliofunika
wawili kwenye Sanduku la Agano. Kerubi pia walijumuisha wenye uhai wanne. Hata
hivyo, walikuwepo wawili tu, Kerubi mwenye kichwa cha mwanadamu na kerubi
mwenye kichwa cha simba, kwa upande wa nje ya Hekalu la nabii Ezekieli kwa ama
upande wa mti wa Mtende ambaye ni Kristo (Ezekieli 41:19). Shetani aliwekwa pamoja na kerubi mlinzi na mtiwa mafuta
kwenye mlima wa Mungu (Ezekieli 28:14).
Ezekieli 28:14-18 Wewe ulikuwa kerubi
mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima
mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. 15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile
ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. 16 Kwa
wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda
dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu
kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe
hayo ya moto. 17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya
uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa
chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. 18 Kwa
wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu
pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami
nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
Hapa tunaona Shetani akiitwa mfalme wa Tiro. Alitupwa
duniani. Alikuwa mpeleka nuru au Lusifa, Nyota ya Asubuhi au Nyota
ya Siku ya sayari.
Isaya 14:12-15 Jinsi ulivyoanguka kutoka
mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa,
Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni
mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za
Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za
kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini utashushwa
mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Hapa huyu Mpeleka Nuru, au Nyota ya Asubuhi alijaribu
kujiinua juu ya Nyota wengine wote wa Mungu na kutaka awe kama Mungu Aliye Juu
Sana. Shetani hakuridhika kule kuwa kwake mmoja kati ya wale Nyota wengine wa
Mungu na Mwana wa Mungu akiwa kama kerubi aliyetiwa mafuta afunikaye. Alitaka
awe kama Mungu Aliye Juu Sana.
Hakuridhika na kuwa kwenye umbo la Mungu, akiwa na umbo
na asili ya kimbinguni, Shetani alitaka kujitwalia haiba ya kuwa sawa na Mungu.
Kwa sababu hii alitupwa hadi chini duniani. Lakini angali bado anaruhusiwa
kweda na kuingia hadi kwenye kiti cha enzi cha Mungu.
Ayubu 1:6 Ilikuwa, siku moja ambayo hao
wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda
kati yao.
Wana hawa wa Mungu walikuwa wameyaasi mapenzi na makusudi
ya Mungu kwa upande mwingine wa gharika kuu kama tunavyoo kwenye Yoshua
24:14-15.
Yoshua 24:14-15 Basi sasa mcheni Bwana,
mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo
baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana. 15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni
hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia
ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi
yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
Uasi ulikuwa ni mchakato endelevu kama tunavyoona kwa
kushirikiana kwao na malaika hawa waasi.
Mwanzo 6:2-4 wana wa Mungu waliwaona hao binti
za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu
milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na
ishirini. 4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku
zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za
binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye
sifa.
Wana hawa wa Mungu walikuwa ni wale Malaika walioasi.
Waliacha makao yao ya kwanza na kufuata tamaa zao mbaya.
Yuda 6-7 Na malaika wasioilinda enzi yao
wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya
milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. 7 Kama
vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa
jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa
kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.
Kristo hakutaka kuwa na usawa wowote na Mungu, bali
aliyatoa maisha yake kwa amri na mapenzi ya Mungu. Tutalielezea vyema jambo
hili hapo chini. Alifanya hivyo ili kuwasuluisha na kuwapatanisha Watakatifu
akiwa kama Kuhani Mkuu.
Melkizedeki alijulikana pia kuwa ni kuhani wa Mungu
Aliye Juu Sana (soma jarida la Melkizedeki (Na. 128)) na
Masihi alijulikana pia kuwa ni kuhani milele wa aina ya
Melkizedeki (Zaburi 110:4; Waebrania 7:1,11). Bwana huyu ambaye ni Bwana
wa Daudi ndiye anayetajwa kwenye Zaburi 110:1 kama ndiye aliyeambiwa aketi
mkono wa kuume wa Bwana hadi hapo atakapowaseta chini ya miguu yake maadui wa
Bwana wa Daudi (Masihi). Huyu Bwana ambaye ni Masihi waliteuliwa na kuwekwa
wakfu na Bwana kuwa ni kama kuhani milele wa aina au mfano wa Melkizedeki. Huyu
anayeitwa Bwana hapa, ni Mungu Baba ambaye ni Bwana wa Masihi na ambaye ndiye
kwa hakika andiko hili ndiye linayomita Masihi.
Kristo au Masihi anajulikana kama Mwana wa Mungu Aliye
Juu Sana kwenye Agano Jipya kwenye Marko 5:7 na Luka 8:28.
Masihi alitwaa mwili wa kibinadamu na kuishi ili
iwezekane kusulibiwa ili kutolewa dhabihu. Hii ilifanywa tena kwenye utoaji wa
dhabihu za hekaluni za Upatanisho wakati kuhani mkuu alipoingia Patakatifu pa
Patakatifu mara moja kwa mwaka na damu ya dhabihu. Masihi alifanya hivyo kama
tunavyoona kwenye waraka kwa Waebrania. Upatanisho huu wa dhabihu ya damu
ilikuwa ni kwa ajili ya kuwapatanisha Watu na Mungu kwa njia ya mpango asilia
wa Mungu ambayo Mungu amewapa Watu wake. Malaika waasi waliikataa njia hii ya
kufikiri na kutenda ambayo ndiyo njia ya Mungu. Kristo hakuwa sawa na Mungu
lakini, akiwa kama Mwana wa Mungu, alikuwa mtiifu. Hii inaelezewa kwenye
Wafilipi 2:6 ambayo ni imepotosha kwenye tafsiri ya KJV. Tafsiri hii ya KJV
inalitaja andiko la aya za 5-7 kama:
Wafilipi 2:5-7 Iweni na nia iyo hiyo
ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye
yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu
kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya
kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Andiko linajulikana sasa kukubalika na wanazuoni wasomi
kuwa halipo sahihi tafsiri yake. Tafsiri ya RSV inasema hivi:
Wafilipi 2:5-7 Iweni na nia iyo hiyo
ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye
yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu
kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya
kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Maana yake ni kwamba kuwa sawa na Mungu halikuwa jambo la
kushikiliwa sana [kama Shetani alivyojaribu kufanya], ambapo kuna maana iliyo
kinyume chake kabisa na tafsiri ya KJV. Neno linalotamkwa arpagmon hapa
lina maana kuwa ni kitendo cha kujitwalia kwa nguvu, ambalo ni uporaji au booty au thamani. Thayer alilisemea hilo
kwenye (ukurasa wa 74) na anafafanua maana ya Wafilipi 2:6 kwenye kipengele
kijulikanacho kama morphe (ukurasa wa 418). Chembe hii ya
hisia ya usawa haikuonekana kama ni kitu cha kushikamananacho au kujivunia sana
kabisa.
Tafsiri ya the American Standard Version inafanya
mrejesho wa tafsiri nyingine ya KJV iliyochapishwa mwaka 1901 ikirudia na
kulisahihisha andiko la Wafilipi 2:6 kusahihisha makosa yaliyofanywa kwenye
Maandiko ya tafsiri ya Authorised Text. Inasomeka hivi:
ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye
hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
Tafsiri nyingine ijulikanayo kama The Jewish New
Testament [Agano Jipya la Kiyahudi] (tafsiri ya David Stern) inasema kuhusu
ayah ii ya 6 hivi:
ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye
hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
Wana wa Mungu wote walichukuliwa kuwa ni malaika au
wajumbe wanaomwakilisha Mungu Aliye Juu Sana. Hakuna walichokifanya kwa mamlaka
au utashi wao wenyewe. Matendo yao yote yalikuwa ni sawasawa na mapenzi ya
Mungu (Luka 11:2; Yohana 5:30).
Yohana 5:30 Mimi siwezi kufanya neno
mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa
sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Elohim wa Israeli alikuwa malaika. Alimtokea
Ibrahimu na alikuwa ndiye Mngu wa Ibrahimu na ndiye alikuwa Mungu wa Ibrahimu
Isaka na Yakobo. Elohim huyu wa Israeli alikuwa pia ni Malaika wa Ukombozi
kama anavyotuambia Yakobo.
Mwanzo 32:1 Yakobo akashika njia yake na
malaika wa Mungu wakakutana naye.
Wakati huohuo alipokuwa akiwasiliana na malaika hawa, na
walikuwa wengi, aliongea na Malaika wa Wokovu akiwa mmoja.
Mwanzo 48:13-16 Yusufu akawaweka wote
wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa
Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa
Israeli, akawasogeza karibu naye. 14 Israeli akanyosha
mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na
mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo
mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza. 15 Akambariki
Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele
zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo, 16 naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki
vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na
Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.
Malaika wa Yahovah (Yehovah) anatambuliwa kama
Masihi na pia kama Elohim na Mwana wa Mungu (soma jarida la Malaika wa YHVH (Na. 024)).
Alikuja kama Mkombozi kwa njia ya kuzaliwa kwake tena duniani. Kwa hiyo yeye
sasa ni kicchwa cha wateule ambao ni watu wa nyumbani mwake Daudi chini ya
Masihi akiwa kama elohim. Zekaria 12:8 inaonyesha kuwa elohim alikuwa pia
Malaika wa Yahovah.
Zekaria 12:8 Katika siku hiyo Bwana
atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa
kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa
Bwana mbele yao.
Malaika wa Bwana anayetajwa hapa ni Yehovah kwenye andiko
hili (soma kamusi ya Green’s Interlinear). Neno Mungu kwenye andiko hili ni
Elohim. Andiko hili linaonyesha kwamba Elohim aliye kwenye maandiko haya
ni Malaika wa Yahovah pia au YHVH na kwamba watu wa nyumbani mwa Daudi
(kwa maneno mengine, wateule) watakuwa kama elohim. elohim.
Elohim aliye kichwa cha nyumba ya Daudi ni Masihi.
Masihi hapa alifanyika kuwa monogenes theos au mzaliwa
pekee wa Mungu aliye kwenye Yohana 1:18. Wakati alipokuwa prõtotokos wa
Wana wa Mungu, elohim, alipokufa alifanyika kuwa mwana wa pekee aliyezaliwa na
hivyo kuwa mzaliwa wa pekee wa Mungu au monogenes theos. Tafsiri
ya the Receptus inamuita monogenes uion au mwana
mzaliwa wa pekee. Kwa jinsi hiyo, alikuwa ni mwana pekee wa Mungu aliyekuwa
anatarajiwa kuzaliwa – kati ya wana wengine wote waliosalia kama roho.
Hatujazaliwa tukiwa kama wana bali ni wana tuioasiliwa wa Mungu.
Kwa hiyo basi inamaana kuwa kuna elohim mkuu na mdogo.
Huyo Elohim mkubwa alijulikana kama Mungu Aliye Juu Sana, au Mungu Mwanyezi
(Mwanzo 14:18-20,22). Kumbukubu la Torati 32:8 inaonyesha kwamba Mungu huyu
Aliye Juu Sana ndiye aliyeyagawa mataifa. Kama tulivyoona, kwa mujibu wa
Maandiko ya kwenye Tafsiri ya the Masoretic Text (MT) ilikuwa ni kwa
mujibu kama ilivyo hesabu ya wana wa Israeli. Hata hivyo, tafsiri ya Septuagint
(LXX) inasomeka kama sawasawa na idadi ya
malaika wa Mungu. Tafsriri ya DSS inaonyesha kwamba maana iliyo kwenye
lugha ya Kiebrania yalisema kuwa sawasawa na (wana wa Mungu) miungu
(au bene Eliym).Israeli alifanyika kuwa ni sehemu ya
Yahova (Yehova). Hii inatupelekea sisi kwenye kutofautisha kati ya
hawa Yehova wawili. Biblia imetanabaisha kwa uwazi sana kuwa kuna Yehova
wawili. Yehova Mliye Juu Sana na Yehova wa Israeli na viumbe wengine wanaobeba
jina na wajihi huu.
Ni kama tulivyojionea hapo juu pia, kamusi ya Strong
inaonyesha tofauti kati ya Yehova Aliye Juu Sana na Yehova wa Israeli. Tofauti
ya kwenye majina ni kwamba Yehovih anatajwa kuwa ni mku na Yahovah anatajwa
kuwa ni mdogo anapotumika peke yake. Wakati neno Yahovah linapotumika kwa
kumtaja yule mkuu, kwa kawaida linajumuisha na anayestahili kama vile
Yahovah wa Majeshi. Idadi sahihi zilizo kwenye kamusi ni zile za SHD 3068
na 3069. Kamusi ya Strong inasema kuhusu Yehovah wa SHD
3068 kwamba lilikuwa ni jina la kitaifa la Kiyahudi au la Wayahudi.
Anasema kuwa jina Yehovah a kwenye SHD 3069 linatumika kwa ajili ya
Adonai [ambaye ni Bwana Yehovih] na linatamkwa na Wayahudi kama Elohim ili
kuzuia kurudiwa rudiwa matamshi hayohayo, kwa kuwa mahali penginepo limetamkwa
kama ilivyo kwenye SHD 3068 kama Adonai wa
kwenye SHD 136 – huyu akiwa ni Mungu.
Hivyo, Wayahudi wanajua kwamba kuna walengwa wawili hapa,
mmoja akiwa mkuu na mwingine mdogo. Kama tulivyojionea, Masihi anajulikana kuwa
ndiye anayeongelewa kwenye Zaburi 45:6-7 ambaye alikuwa ndiye aliyetiwa mafuta
na Mungu wake.
Zekaria 2:3 inaonyesha kwamba Malaika wa
Yahovah (ambaye hapa ni wazi sana kuwa ni Masihi) alimpa ujumbe Zekaria
kuhusu ujio wake katika Israeli kwa maongozi ya Bwana wa Majeshi. Tofauti
inaonekana wazi sana kwamba tunaomungelea Masihi na Mungu Baba ambaye ni Bwana
wa Majeshi.
Zekaria 2:8-12 Kwa maana Bwana wa
majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka
ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake. 9 Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao
watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi
amenituma. 10 Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana,
tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema Bwana. 11 Na
mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu;
nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako. 12 Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi
takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena.
Tofauti iliyopo kati ya Yahovah wa Israeli anayeitwa
elohim na eloim wake anayeitwa Eloah au Mungu Mwenyezi. Bwana wa Majeshi,
ni tofauti ambayo imepotea kwenye lugha ya Kiingereza ambako kuna jina linguine
la Mungu. Nia yake haijaanikizwa bado kwa wasomaji wake.
Masihi atawarithi Yuda wakiwa ni sehemu na milki yake
katika nyakati za mwisho. Atauchagua tena Yerusalemu atakaporudi mara ya pili.
Harakati hizi za Masihi zaweza hatimaye kuparaganyikia mbali kwenye migawangiko
kwa mkururu.
1. Tukio
la kuzaliwa kwake tena hapa duniani (soma mkururu wa majarida yaliyoorodheshwa
kwenye Programu ya Mafundisho ya Biblia (Na. B1)).
2. Mkururu
Mwandamamo wa Makanisa (soma jarida la Nguzo za Filadelfia (Na. 283).
3. Nyakati
za Mwisho (soma majarida ya Jeshi la Gideoni na Nyakati
za Mwisho (Na. 022); Maonyo ya Nyakati za Mwisho (Na. 044); Vita na Mapigano ya Nyakati za Mwisho na Vitasa vya
Hasira ya Mungu (Na. 141B); Siku ya Bwana na Nyakati za Mwisho (Na. 192); Miaka Thelathini ya Mwisho: Pambano la Mwisho (Na. 219); Mpingakristo Kwenye Teolojia ya Kanisa la Kwanza na
Nyakati za Mwisho (Na. 299F).
4. Kurusi
kwa Masihi (soma jarida la Kurudi kwa Masihi: Sehemu va
I (Na. 210A)).
5. Milenia
(sawa pia na jarida la Milenia na Unyakuo (Na. 095)); Yubile ya Dhahabu na Milenia (Na. 300).
6. Hukumu
(soma majarida yaliyoorodheshwa kwenye mkururu wa Programu ya Masomo ya Biblia (Na. B1)).
7. Mji
wa Mungu (soma kwenye jarida la Mji wa Mungu (Na. 180)).
Jarida hili linatumika kama utangulizi wa mkururu wa
majarida yenye kichwa hiki cha maneno ambayo mengi yake yamehesabiwa na
kujumuishwa ndani yake.
q