Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[076B2]
Kristo na Malaika Mkuu Mikaeli
(Toleo La 1.0 06072013-06072013)
Elohim wa Israeli aliye kwenye maandiko ya Agano la Kale hakujulikana kuwa
ni Mungu wa Pekee wa Kweli wala kuchukuliwa kuwa ni huyo kabisa. Bali zaidi tu
ni kwamba alichukuliwa kama elohim msaidizi ambaye yeye mwenyewe alikuwa ni
elohim ambaye Mungu alikuwa juu yake huyo Eloah. Kiumbe huyu na Mungu wake
Eloah wanaonyeshwa kwa wazi kwenye maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya, na
kudai vinginevyo ni upotoshaji mkubwa sana na wa makusudi.
Christian Churches of God
PO Box 369,
WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Hatimiliki ă 2013 Wade Cox)
(tr. 2017)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na
tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji
kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa
toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya
sheria ya hati miliki.
Masomo haya
pia yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Kristo
na Malaika Mkuu Mikaeli
Kenye makala yake ijulikanayo kama Question and Answer Section, [Makala ya
Mwaswali na Majibu] (Toleo la Julai-Agasti 2013 | Jarida la Tomorrow’s World [Ulimwengu wa Kesho]), Kanisa
liitwalo the Living Church of God lilichapisha swali la aina ya Dorothy Dix ambalo
lilihusika na masuala nafasi ya Kristo kwenye Agano la Kale. Liliacha kwa
kitambo kuficha ukweli wa teolojia yao ya Kiditheism (soma jarida la Uditheism (Na. 76B)); na
madai yao kwamba Kristo alikuwa ndiye yule Mungu wa Agano la Kale na kwamba
Baba hakudhihishwa kwenye Agano la Kale. Madai haya
ni ya uwongo kabisa kama tutakavyoona huko mbele.
Mhariri anaanza kwa kuuliza Swali linaloonekana kuwa liliandaliwa ili
kupinga habari kwamba kama Kristo anatajwa kwenye Agano la Kale ndipo atakuwa
ni Mikaeli akiwa ni kiumbe aliyekuweko akiishi kwenye kipindi cha kabla ya
kuzaliwa kwake rasmi duniani. Ukweli ni kwamba, jina la Mwana wa Mungu
lilipaswa litangazwe kama tunavyoona kutoka kwenye swali lililo kwenye Mithali 30:4
ambapo panasema: Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni
nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya
nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni
nani jina la mwanawe, kama wajua?
Jina la Mungu Mmoja wa Kweli limetolewa kwenye aya hiyohiyo inayofuatia ya
5. Kila neno la Mungu limethibitishwa... na neno lililotumika kumtaja Mungu
kwenye Kiebrania ni Eloah ambalo ni
la umoja na inakubali kutokuwa na uwingi kwa namna yoyote ile. Jina la Mwana
yapasa liwekwe au liingizwe pahala pengine. Tunaweza sasa kulitafakari jibu lao
kwenye swali hili.
Je, unapajua mahala unapoweza
kumkuta Yesu Kristo kwenye Agano la Kale?
Swali: Mchungaji wa rafiki yangu
anasema kuwa malaika mkuu Mikaeli ni roho yuleyule mwenye mwonekano wa kimwili
kama alivyokuwa Yesu Kristo. Biblia inasemaje hasa kuhusu ujulikano wa Mikaeli
na Kristo?
Jibu: Madhehebu
yanadai kimakoa au kwa
upotoshaji mkubwa kwamba Yuda 1:9 inamrejekea au kumtaja Yesu Kristo pamoja na
rejea au kumtaja “Malaika Mkuu” anayejulikana
kama Mikaeli. Mawazo yao ni kwamba neno hilo ambalo kwa Kiyunani huandikwa archaggelos
kwa maana ya “malaika mkuu,” ni la umoja, kwa hiyo ni lazima liwe
linarejelea au kutaja uwepo wa malaika mmoja
aliye mkuu na mwenye mamlaka makubwa ya aina zake. Na ndipo wanapoihusisha
aya hii na ile ya 1 Wathesalonike 4:16—kuna moja tu nyingine ya kwenye Agano
Jipya hutumia neno hili archaggelos—ambayo inasema, "Kwa sababu
Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika
mkuu, na parapanda ya Mungu." Mawazo na nadharia hii ni ya makosa na upotoshaji, kwamba je, kurudi kwa
Kristo kwa hiyo ni lazima kuambatane na roho hiyohiyo ya mwonekano wa kimwili
kama ya malaika Mkuu Mikaeli.
Ni kweli,
kumuelezea malaika mkuu kama anayeshuka kutoka juu au mbinguni “akiwa na sauti
ya malaika mkuu” kunafanya iwe ni kama inaeleweka au kukubalika kama kumwelezea
mtu mwanaume akiimba “pamoja na sauti ya mwanaume.” Kwa namna nyingine, kama
mwimbaji alikuwa na nguvu nyingi sana kuliko sauti nyingine inayojulikana,
zaidi ya uezo wa kibinadamu, lingekuwa ni jambo la kiasilia kulinganisha nguvu
zake na kwa sauti kubwa zaidi ijulikanayo. Hivi ndivyo sasa tunavyoweza
kuyaelewa vizuri zaidi maneno ya Mtume Paulo yaliyo kwenye 1 Wathesalonike
4:16.
Ni Malaika wake? Hoja zingine
zilizopangiliwa kimakosa au kiupotoshaji zinadhaniwa kuwa iwapo kama Ufunuo 12:7
inamwelezea Mikaeli na jeshi la “malaika wake” wakipigana na Shetani (Joka), basi
ni lazima Mikaeli awe ni kiongozi wa jeshi hilo, na ni lazima atakuwa na haiba
sawa nay a Yesu Kristo, ambaye Maandiko Matakatifu mahali pengine yanamwelezea
kama ni kamanda wa malaika wenye nguvu nyingi.
Hii, pia, ni dhana na nadharia potofu. Kila jeshi lina madaraja ya vyeo na ngazi
mbalimbali, kama vile sajenti na jenerali ambao wote wawili wanaweza kuliita
kundi la maaskari “watu wangu.” Mikaeli naye akiwa na “malaika wake”
hakumjumuishi tena Mikaeli kutoka kuwa ni mmoja wa malaika aliye chini ya Yesu
Kristo! Jaribu kufikiria, pia, maana ya vita ya Mikaeli. Maandiko Matakatifu
yanamwelezea Mikaeli kama anayepigana na joka na malaika zake! Ndiyo, Shetani ana “malaika zake” na siye Yesu Kristo! Na ni
vivyohivyo alivyo Mikaeli! Shetani alishagawahi kuwa mfalme wa malaika wote—wakati
alipokuwa mkamilifu katika njia zake zote
(Ezekieli 28:14–16)! Kuwepo kwake akiwa kama Lusifa mleta nuru au mwenye
mng’aro, Nyota ya Mchana (nyota likiwa ni jina lingine la malaika na mjumbe kwa
Kiebrania), akimweka yeye sio mahala pengine popote bali pa chini zaidi kuliko
kuwa ni malaika mkuu mwenye nguvu au
“kerubi afunikaye.”
Maandiko
Matakatifu yameweka wazi kwamba hakuna malaika aliye zaidi ya kuwa mtumishi.
Malaika hawapasi kuabudiwa wala kuombwa (Wakolosai 2:18, Ufunuo 22:8–9), na wana
kikomo cha kiuweza. Wote wawili, yaani Mikaeli na Kristo walikuwa viumbe, na
kama tungali waona tusingeiona tofauti kubwa sana kati yao na hata kwa jinsi
walivyoshughulika na Shetani. Kumbuka kwamba Mikaeli alikataa kumkemea Shetani
kwenye waraka wa Yuda 1:9—ni tafauti na ilivyokuwa kwa makemeo makubwa
aliyoyafanya Yesu Kristo akimkemea kama tunavyoona kwenye Luka 4:8! Kumbuka pia
kwamba Yuda anamtaja Yesu Kristo moja kwa mojakwenye Yuda 1:1 na Yuda 1:17. Kwa
namna nyingine anaunganisha na aya yake ya 9 inayomwelezea au kumtaja Mikaeli pamoja
na rejea nyingine yeyote inayomtaja Yesu Kristo. Anawachukulia wao kuwa ni kama
viumbe wawili tofauti—ambao ni pamoja na walivyo wao!
Ule Mwamba Ulikuwa ni Kristo! Kwa hiyo basi, hivi alikuwa wapi Yesu
Kristo kabla hajaja hapa duniani? Maandiko Matakatifu yanaeleza kwamba
Neno—Logos—alikuwa Mungu, na alikuwa pamoja na Mungu Baba tangu milele yote (Yohana
1:1). Huyu Neno hakuwa ni malaika aliyeumbwa. Kwa kweli, alikuwa ni Neno—na
siyo Mungu Baba—ambaye Waisraeli wa hapo zamani waliyefuatananaye (1 Wakorintho
10:4). Yesu Kristo aliwaambia Waisraeli kinagaubaga kabisa kwamba hawakumjua
bado Mungu Baba—bali ni Kristo tu ndiye aliyemjua yeye—na ilikuwa ni Yesu Kristo
ambaye ndiye angemdhihirisha Baba kwao (Yohana 1:18; 17:25)! Hakuna malaika wa
kawaida angefaa kukubalika sadaka yake kwa ajili ya wenye dhambi; bali ni Mwana
wa pekee wa milele wa Mungu tu, ndiye angefaa na kustahili kulijaza pengo hilo.
Mtoto au Mwana huyo ni Yesu Kristo. Maandiko Matakatifu yanaeleza na
kudhihirisha wazi sana kwamba Mikaeli malaika mkuu ni kiumbe aliyeumbwa ambaye
anatumika na kuhudumu chini ya Kristo.”
Michanganuo hii
inaangukia kwa kuhusiana na ukweli wa kwamba Kristo anatajwa rasmi kabisa kuwa
ni kama nyota ile itakayokuja kutoka kwa Yakobo (Hesabu 24:17) ambaye ndiye Israeli
na Yuda kwenye unabii ulio kwenye Torati. Hata hivyo, wakati kunapokuwa na hawa
“wanazuoni” waoga.
Rejea iliyo kenye
Yohana 1:18 inaangukia kushughulikia ukweli wa kwamba Kristo alikuwa ni monogenes
theos ambayo maana yake ni ni theos mzaliwa wa pekee au mwenye
mamlaka ya Mungu na aliye kifuani mwa baba na alitangazwa au kunena. Kwa hiyo
alikuwa ni malak au mjumbe (soma jarida la Kwenye Maneno: Monogenes Theos Kwenye Maandiko Matakatifu na Mapokeo (Na.
B4)). Haikuwa
ni muda kitambo sana uliopita kwamba watu hawahawa walikuwa wanalitumia andiko
hili ili kueneza mafundisho ya Utatu na kukataa umuhimu wake na maana yake.
Kumbuka kwamba
imeonyeshwa vizuri sana kwamba Kristo alikuwa ni kiumbe aliyekuwa pamoja nao
jangwani na ilikuwa ni yeye aliyeonekana kuwa ni malaika wa uwepo wake ambaye
ndiye aliyemkabidhi torati Musa pale Sinai. Wanalazimishwa kuukubali ikweli huu.
Uwepo wa Yesu Kristo katika kipindi cha kabla ya kuzaliwa kwake rasmi duniani
imeelezewa kwa kina kwenye jarida la Uwepo wa Yesu Kristo Kipindi cha Kabla ya Kuzaliwa
Kwake Rasmi Duniani (Na. 243).
Kumbuka pia
kwamba kuna maandiko mengi sana yaliyoachwa nje ya mfano huu yanayoonekana
kuyakanganya Maandiko Matakatifu na kuendeleza mafundisho ya kizushi ya Kiditheist
na madai ya uwongo na mapotofu kwamba Mungu Baba hakuwa anajulikana tangu
kwenye Agano la Kale.
Kumekua kila mara
ikifundishwa kwenye imani za Kisabato kwamba Kristo aliitwa mahali
penginepopote kwenye Agano la Kale kuliko jina lile basi atakuwa Mikaeli. Hayo
ndiyo yalikuwa ndiyo mafundisho ya imani ya SDA hadi pale ilipojitangaza kuwa
imegeukia rasmi imani ya Utatu au Utrinitarian mwaka 1978. Lilikuwa ni fundisho muhimu na linaloainisha
imani yao kwao, pamoja na yalivyokuwa Makanisa lingine linalojulikana kama
Kanisa la Mungu la Siku ya Saba maarufu kama Churches of God (Seventh Day) ambako
ndiko walikoyachukua mafundisho haya, kwamba Malaika Mkuu wa Agano la Kale
alikwa ni Mikaeli, na kwamba kiumbe huyo alikuwa ni Kristo. Kanisa la WCG, na machipukizi
yake (isipokuwa kwa baadhi yake tu) ndiyo hayakuyaendeleza mafundisho haya hata
kwa pale walipoanzisha na kuingiza teolojia potofu kutoka kwenye Uditheism “Mafundisho
Mapotofu ya Yakizushi ya Nguvu Mbili za Kiuungu” ambayo baadae ilichukuliwa na
kuingizwa kwenye Ukristo yaliyotafuta kudai kwamba kulikuwa na viumbe wawili
walio miungu wenye haiba sawa kwa umilele na kwa kila kitu na ambao walikuwepo
kabla ya uumbaji na mmoja wao aliaamua na kuhiyari kuja hapa duniani na kuwa ni
mwana wa mwingine. Haya siyo mafundisho ya kukubalika kwenye imani ya Kikristo
bali yalichukuliwa kutoka kwenye teolojia ya Kibinitarian ya dini potofu za
waabudu mungu Jua Attis wa Roma na Adonis na Orisis wa pande za Mashariki mwa Mediterranean
na kutoka kwa Mithras na Baali kwenye dini nyingine potofu ya waabudu jua wa huko
Asia Ndogo. Mwenzi wake alikuwa ni mungumke mama aliyejulikana kama Easter au
Ishtar au Cybele au Isis au Ashtarothi mwenzi wa Baali. Mafundisho haya
yalichukuliwa kutoka kwa waabudu Baali na yalilaaniwa na kukatazwa kwa nguvu zote
kwenye Biblia.
Kanisa la LCG na
makanisa mengine yaliyochipuka pamoja nalo yamekuwa yakiyapuuza kwa makusudi
kabisa maandiko mwongozo ya Biblia yanayoonyesha kwa wazi sana kwamba malaika
wote ni wana wa Mungu na kwamba Shetani naye ni mwana wa Mungu. Ayubu 1:6 na
2:1 zinaaonyesha kwamba wote hao walikuwa wanaruhusiwa kwenda kwenye kiti cha
enzi cha Mungu pamoja na Shetani na alikuwa na fursa kama hiyo ya kutembelea katika
kipindi cha Ayubu ambaye alikuwa ni mkazi wa eneo la Isakari katika Mashatiki
ya Kati (huenda ni huko Midiani). Wana hawa wa Mungu walikuwa elohim ambao
walikuwa ni jeshi kubwa la malaika na walijulikana kama hivyo na wanazuoni au
wasomi wa Biblia kama vile Bullinger na wengineo. Wana wa Mungu waliitwa elohim
ambalo ni neno la umoja linalommaanisha Mungu kama ni kiumbe mwenezi. Elohim
ametajwa kwenye Ayubu 2:1 lakini jina Eloah limetumika mara nyingi likimtaja na
kumaanisha Mungu wa Pekee na wa Kweli kwenye kitabu chote cha Ayubu. Ayubu 1:6 inamtaja
Shetani kuwa ni miongoni mwa wana wa Mungu. Kwa hiyo anatumika kumjaribu Ayubu
na kumtesa. Ayubu 2:1 pia anamwonekano huohuo wakati wana wa Mungu walipojihudhurisha
mbele za Mungu na Shetani alikuwa pamoja nao miongoni mwao. Kwa hiyo hakuna
mashaka babisa kwamba kulikuwa na wana wengi wa Mungu katika nyakati za Agano
la Kale na Shetani alikuwa ni miongoni mwao na wote waliruhusiwa kujongea
kwenye kiti cha enzi. Wana hawa wa Mungu waligawanyika kwenye vyeo au madaraja
na tunaona kwenye Ayubu 38:4-7 kwamba Mungu Mmoja wa Kweli aliiumba dunia hapo
mwanzoni na kwamba wana wa Mungu walijihudhurisha mbele za Mungu muumbaji na
Nyota wote wa Asubuhi waliimba kwa furaha wakati walipooonyeshwa uumbaji. Kwa
sasa, huyu Nyota wa Asubuhi ndiye mtawala wa ulimwenhu na anatajwa na
kujulikana kama mpeleka nuru au “Lusifa”
na hawa viongozi wa Jeshi la Malaika wa Mbinguni walikuwa ni watawala wa Baraza
la Mbinguni ambalo tulionyeshwa pale Sinai waliwa wameanzishwa tena kwenye
Maskani kama baraza lililojulikana kama Sanhedrin la watu au wajumbe Sabini
jumlisha Wawili, na ambaye waligawanyika kwenye Baraza la Mbinguni la kwenye
Ufunuo sura za 4 na 5 la Makerubi Wanne na lenye Wazee Ishirini na nne na Mwana
Kondoo wa Mungu. Baraza la nje lilikuwa na wazee wengine ishirini na wawili
wakifanya jumla ya wanabaraza 72. Hili ndilo lilikuwa baraza la Sanhedrin pia la
kutoka Sinai na la wanabaraza Sabini na wawili au Hebdomekonta [Duo] lililoanzishwa
na Kristo na wazee wa kanisa (Luka 10:1,17).
Sasa wana wengi
wa Mungu walitumwa kwa wanadamu kama wajumbe na kwamba neno lenyewe lilikuwa Malak kwa Kiebrania na kwa Kiyunani aliitwa
Aggellos. Neno hilo lilimaanisha tu
mjumbe na elohim walikuwa wote wana wa Mungu kama elohim hadi walipotumwa kwa
wanadamu wakiwa kama malak. Na ndiyo sababu
wote waliitwa kama Yahova na jeshi la kibinadamu walionyeshwa mbele zao (Gr. proskuneo). Neno hilohilo limetumika kwa
wateule wakati wale wanaosema kuwa wao ni Wayahudi bali siyo lakini wakituama
kwenye proskuneo mbele za wateule wa Kanisa la Wafiladelfia kwenye Ufunuo 3. Waumini
wa imani ya Kibinitarian waliomuabudu mungu Attis huko Roma walileta mafundisho
yao potofu ya kizushi na kuyaindiza kwenye Ukristo tangu mwaka 175 BK. Ili
kuiingiza kwa imani ya Kibinitarian ya mungu Attis iliwalazimu kumuinua juu na
kumtukuza Kristo kwenye kiwango cha juu na kumfanya aonekane yuko juu zaidi
kuliko wana wengine wote wa Mungu au elohim. Walilifanya hilo kwa kuunda daraja
na kuwaita wao kuwa “Malaika” kutokana na neno aggellos au mjumbe ambayo ilikuwa ni tafsiri ya neno malak au mjumbe kwenye Agano la Kale. Na
kwa hiyo waliwafanya watofautiane na Kristo na wakalitumia neno elohim au theos
wa yeye na Baba peke yake. Wakiwa wamefanya upotoshaji huu ndipo walimjumuisha
Roho Mtakatifu kuwa ni kama wa tatu kwenye mjumuiko huu wa Mungu wa Utatu mwaka
381 BK kwenye Mtaguso wa Constantinople na kuthibitisha au kuupa nguvu kwenye
Mtaguso wa Kalkedon mwaka 451. Mchakato wenyewe na teolojia yake vimeainishwa
kwa kina kwenye jarida la Upotoshaji wa Wabinitarian na Watrinitarian Kuhusu Teolojia ya Mwanzon ya
Uungu (Na. 127B).
Tunajua kwamba Jeshi
la Malaika wa Mbinguni liligawanyika kwa makundi 72, kama mataifa yalivyoorodheshwa
kati ya zama za kale na kuwa sabini na mbili na waligawanyika sawasawa na idadi
ya wana wa Mungu. Hii imeandikwa au kuorodheshwa kwenye Kumbukumbu la Torati 32:8
(soma tafsiri za RSV na the DSS na the LXX ambamo neno elohim limetafsiriwa kuwa
Aggellou Theou), na andiko lililo kwenye Sura ya 32 lilimwonyeshwa Eloah kuwa
ni Mungu linashangaza sana. Ni andiko hili ndilo linamwonyesha elohim kuwa
ndiye anayewapatia milki Israeli wakiwa ni urithi wake ambaye pia anatajwa kama
Yahovah wa Israeli. Huyu ndiye
elohim ambaye alishinana kwa mweleka na mababu wa imani na aliyenena na
Ibrahimu na Hajiri. Andiko la Kumbukumbu la Torati 32:8 liligeuzwa maana na
kupotoshwa na baraza la Sopherim ili kuepuka ukweli wa kwamba Yahovah aliyewamilikisha
nchi Israeli alikuwa ni elohim mdogo aliyetajwa na kumaanishwa kwenye Zaburi
45:6-7 na ameelezwa au kuoneshwa kwenye Waebrania 1:8-9 kuwa ni Yesu Kristo. Upotoshaji
huu wa kugeuza maana halisi iliyokusudiwa ulifanyika mara 134 kwenye Agano la
Kale na jopo la Sopherim. Zaburi
inalitaja pia baraza la elohim na Zaburi 82:6 inasema kuwa wao wote ni Miungu.
Kristo anajitaja mwenyewe kama mmoja wa elohim hawa kwenye Yohana 10:34-36 na ndiyo
sababu iliyowaghadhibisha hata wakamuua na walipotosha maana ya andiko la Agano
la Kale ili kuficha ukweli huo. Andiko lililo kwenye Danieli linamuonyesha wazi
kabisa Mikaeli kuwa ni kama Mfalme Mkuu asimamaye
kwa niaba ya taifa la Israeli na kwamba kwa kuwa Kristo ni Mwana wa Mungu
aliyetajwa kwenye Agano la Kale, ambaye Mungu anampinga mtu yeyote anayedai
kuijua sana Biblia na kutangaza, jina lake ni Mikaeli kama tunavyoona kwenye
Danieli 12:1 na penginepo. Hivi ni vita vya Nyakati za Mwisho wakati
atakapotumwa aje kuwakomboa Israeli. Hii Zekaria 2:8-13 ambako Yahova wa Majeshi,
Mungu Mmoja wa Kweli, Elyon, anapomtuma Yahova wa Israeli huko Yerusalemu na
kwa mataifa yaliyowapotosha, kwa kuwa yeye augusaye Yerusalemu anaigusa mboni
ya jicho lake [inasomeka jicho langu]. Huyu Mungu Mmoja wa Kweli aliyetajwa
kwenye Agano la Kale kama Eloah, na pia kwa mwandiko wa Kikaldayo Elahh. Yeye
ndiye anayestahili kuabudiwa na kutolewa dhabihu za Hekaluni na ndiye ambaye torati
na sharia zinatoka kwake (Ezra 4:23-7:26). Neno Yahova ni la nafsi ya tatu ya
vebu yenye maana ya “anasababisha iwe” linalotokana na Kutoka 3:14 ‘eyeh ‘asher
‘eyeh maana yake ni Nitakuwa kama Nitakavyokuwa (soma pia tafsiri ya Annotated Oxford RSV). Kwa hiyo Eloah alifanyika
Ha Elohim au Mungu kama kichwa au kiongozi wa kiumbe jumuishi.
Tunawezaje kujua
kwa hakika kwamba elohim ambaye alikuwa Mungu wa haraka wa Yakobo alikuwa malak au aggellos (LXX) aliyemkomboa yeye, na mababa wengine wa imani kama
Ayubu. Ni kwa sababu tu tunaambiwa kwamba ilikua ndiyo ilivyokuwa kwa Yakobo na
pia kwa Ayubu na kwa Musa, aliyeandika vitabu vyote viwili, cha Ayubu na cha
Mwanzo. Kwenye Mwanzo 48:15-16 tunasoma habari ya Yakobo akiwabariki Efraimu na
Manase na ndiye Yusufu akisema:
15 Akambariki
Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele
zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo, 16 naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki
vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na
Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.
Bilashaka kwamba
elohim huyu alikuwa ni malak au aggellos (LXX) kama ni ombi kwa kiumbe mmoja
anayebariki barobaro na siyo viumbe. Huyu malak au mjumbe alikuwa ni elohim
akiwa kama mmoja wa wana wa Mungu. Tunaona pia kwamba yeye ni kichwa au
kiongozi wa watu wa nyumbni mwa Daudi na Israeli kwenye Zekaria 12:8 na wote
wakafanyika kuwa elohim. Ayubu anasema pia kwamba mwokozi wake alikuwa ni mmoja
wa watu wakuu wa elohim ambao wanafikisha idadi ya viumbe 1000 (Ayubu 33:23-24).
Elohim wa Israeli aliye kwenye Zaburi 45 pia alikuwa elohim wake juu yake
ambaye alikuwa ni Mungu Mmoja wa Kweli na kiumbe huyo alimuinua na kumtukuza
yeye zaidi ya nafasi waliyonayo ndugu zake wote ambao nao walikuwa washiriki
kwenye baraza la elohim wa kwenye Zaburi. Huyu elohim mdogo alikuwa ni Kristo (Waebrania
1:1-9).
Kwa hiyo
haiwezekani kabisa kwa maandiko ya Agano la Kale kudaiwa kuwa hayamtaji wala
kummaanisha Mungu Mmoja wa Kweli na kuonyesha kwamba mmoja wa wana wa Mungu ni Yahova
mdogo wa Israeli na ndiye inayomjata Biblia kuwa ni Yesu Kristo. Kwahiyo imethibitika
kwamba huduma ya lililokua kanisa la WCG na kamanisa mengine yaliyoparaganyika
kutoka humo hayajui tu wanachokisema. Wanahubiri mafundisho ya uongo na
mafundisho ya miungu ya uwongo na kwa ukweli huo ndiyo maana hawakuachiliwa pia
washike na kuifuata Kalenda Takatifu kabisa. Na wala hata Herbert Armstrong hakuachiwa
afanye hivyo, aliyewafundisha wao mafundisho haya ya uwongo na mapotofu, bali
yeye pamoja na wao hawakuelewa kikamilifu kilichokuwa cha kweli na kwa hiyo
ndipo walishimdwa kufundisha vizuri na kiusahihi.
Majina ya Kristo
Kwa kuongezea majina
ya Elohim wa Agano la Kale ndipo pia tuna majina mengine aliyoitwa Kristo
kwenye Agano Jipya. Injili inamuita yeye kuwa Immanueli ambaye maana yake ni
“Mungu pamoja nasi” na wala hakuitwa hivyo kabisa licha ya kuelekezwa na
malaika. Aliitwa Yahoshuah aur Joshua kwa Kiingereza (Yoshua kwa Kiswahili) au
“Yahovah anaokoa” (au wokovu wa Yaho[vah]) ambalo lilikuwa ni jina la mwanadamu
aliyenena na jemadari wa jeshi la Bwana huko Yeriko, aliyeitwa Yoshua mwana wa
Nuni, maana yake ni “Wokovu wa Yahova huka kwa njia ya uvumilivu.” Majina
mengine ya kinabii ya kwenye Agano la Kale yanapatikana kwenye jarida la Isaya 9:6 (Na. 224). Majina mbalimbali yanayomhusu Masihi kwenye maagano yote mawili yaani
kwenye Agano la Kale na kwenye Agano Jipya yanaonyesha kwamba kuna mabadiliko
kwenye daraja lake la kicheo kwa namba zote mbili, elohim na malak au aggellos/aggellos
mkuu na kama Mwana wa Adamu na majina yenyewe yanabeba maana kama hiyo.
Andiko la kwenye
waraka wa Yuda linaonyesha wazi Kristo na imani
waliyopewa watakatifu mara moja tu kuwa ni kama msisitizo au kiini kikubwa
cha andiko lenyewe na andiko la Mikaeli na Shetani linaonyesha kwamba alikuwa
ni Mikaeli aliyewaongoza mle jangwani huko Yordani mkabala na Yeriko aliyepigana
na Shetabi akiugombea mwili wa Musa na alikuwa ni Mikaeli huyu ndiye
aliyekutana na Yoshua huko Gilgali akiwa kama jemadari wa majeshi ya Bwana (soma
pia jarida la Kuanguka kwa Yeriko (Na. 142)). Huyu ni mfalme mkuu anayesimama kwa niaba ya
watu wa Israeli na kama Kristo ametajwa kwenye maandiko ya Agano la Kale kama yanavyosema
maandiko ya kitabu cha Mithali kwamba alikuwa ni Mikaeli. Yeye ni malaika mkuu
wa Jeshi la Mbinguni akiwa mkuu kwenye komandi na cheo cha Malaika. Soma pia
kwenye jarida la Yoshua, Masihi, Mwana wa Mungu (Na. 134).
Makanisa ya LCG na
UCG na mengine yanayomwabudu Armstrong na kushikilia itikadi zake hayawezi
kumudu kukubali kwamba Armstrong alikosea ni kama kwakweli ilivyo vita kwa
kujilimbilikizia au kujipatia fedha tu kwa sasa na siyo kwa ajili ya ukweli.
Wangeweza hatimaye kukubalia makosa ya kimafundisho kuhusu Tabia na Asili ya
Mungu na kisha kuhusu Kalenda.
Wao wawajui vya
kutosha. Wengi wao hata ni bado Waprotestanti ambao hawajaongoka; ambao hukumu
imekuwa ikitolewa na Armstrong kwa Waprotestanti hao ambao haakuwa wanaelewa
vizuri Asili ya Mungu kama ilivyoelezewa kwenye maandiko kadhaa wa kadhaa ya
Biblia.
q