Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[CB33]

 

 

 

 

Sikukuu ya Pasaka na Mikate Isiyotiwa Chachu

(Toleo La 2.0 20030612-20070125)

Mara tatu kwa kila mwaka Wakristo wameamriwa kutoka nje ya makazi au nyumba zao na waende wakakusanyike pamoja mahali atakapolikalisha Bwana jina lake ili wakazishike huko Sikukuu alizowaamuru Mungu. Idi ya Pasaka na Mikate Isiyotiwa Chachu ni maadhimisho ya kwanza kati ya Sikukuu hizi tatu.

 

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

 (Hati Miliki © 2003, 2007 Kellie Elson, ed Wade Cox)

(tr. 2014)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 


Sikukuu ya Pasaka na Mikate Isiyotiwa Chachu




Swali: Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu Ni nini?

 

Ni mojawapo ya Sikukuu kubwa ambazo Bwana Mungu wetu aliamuru tuziadhimishe kwa kwenda huko kila mwaka, tunapokuwa tunakusanyika pamoja nje ya nyumba zetu na kuyafanya yale anayotuamuru kuyafanya. Tunaukumbuka wakati huu kuwa ni ule ambao Mungu aliwatoa wana wa Israeli kutoka utumwani Misri.

 

Swali: Kwa nini hatuketi majumbani mwetu tunapoishika Sikukuu Hii ya Mikate isiyotiwa Chachu?

 

Kumbukumbu la Torati 16:5-6 Usimchinje pasaka ndani ya malango yako yote akupayo Bwana, Mungu wako; 6 ila mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinja pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri

Swali: Kwa nini tunakula vyakula Visivyotiwa Chachu ndani yake?

 

Mungu anatuambia kwamba tusile kitu ch0chote chenye chachu au hamira wakati huu wa maadhimisho ya Pasaka.

 

Kutoka 12:17-20  Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. 18 Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni. 19 Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. 20 Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote  

 

Hapa Bwana anatuambia anatuambia kuadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Anatuambia pia wakati unaopaswa kuiadhimisha. Mwezi wa Kwanza wa mwaka mpya unaitwa mwezi wa Abibu. Maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka yanaanza tangu siku ya 14 ya mwezi wakati wa jioni na inaendelea hadi siku ya 21 ya mwezi wakati wa jioni. Hii ni Sikukuu ya siku saba na tunakusanyika katika jioni au usiku wa siku ya 14 ili kuja kusherehekea na kuadhimisha Ushirika wa Meza ya Bwana. Tangia siku ya 15 hadi siku ya 21 ni Siku Takatifu. Tunazitakatifuza siku hizi sawa na kama tunavyoadhimisha na kuzitakatifuza Sabato za kila juma. Kwa hiyo, tutakula mikate isiyotiwa chachu kabisa kwa muda wa siku saba. Tujihadhari kutokula kitu chochote chenye chachu au hamira ndani yake. Hamira ni mseto ili kuifanya iumuke. Hii inaashiria au dalili ya vitu anavyovitumia Mungu ili kutufundisha kwamba sisi hatujakamilika pasipo yeye. Hii ni namna inayoashiria dhmira ya kuondoa dhambi au kuachana na dhambi maishani mwetu.

 

Tumeelekezwa ama kuamriwa kufanya hivyo kwa vizazi vyetu vyote milele. Hii inamaanisha kuwa wazazi wanapaswa kuiadhimisha, kisha watoto nao wanapaswa kuiadhimisha na hara watoto wa watoto wao waendelee kufanya hivyo vizazi vyao vyote. Ni muhimu kwa watoto kushiriki kwenye maadhimisho ya Pasaka ili wasikilize na kujifunza yanayofanyika na kwa nini inafanyika hivyo, ili kwamba kipindi chao kikifika wayakapokuwa watu wazima wapate kuyajua majira au wakati, sababu na sababu ya kufanya maadhimisho haya.

 

Swali: Kwa nini tunaidhimisha Pasaka?

 

Kutoka 12:14  Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele

 

Tunaiadhimisha Pasaka kwa kuwa Bwana Mungu wetu ametuamuru kufanya hivyo.

 

Ukumbusho maana yake ni kipindi tunachoakumbuka na kuadhimisha au kusherehekea kitu fulani likiwa kama ni tukio maalumu la namna fulani. Pia katika kipindi hiki tunakumbuka kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na baada ya siku tatu za usiku na mchana za kuwepo kwake kaburini alifufuka kutoka kwa wafu na kwenda kwa Baba, Mungu wa Pekee na wa Kweli (Eloa). Kumbuka kwamba dhabihu ya Yesu Kristo iliyolewa kwa ajili ya dhambi zetu. Tunapaswa mara zote kuiadhimisha Sikukuu hii na kuhakikisha kuwa tunawafundisha watoto wetu. Amri hii haiwezi kusamehewa kwa anayeivunja. Mungu alituamuru kuiadhimisha Pasaka milele!

 

2Wafalme 23:21 Mfalme akatoa agizo hili kwa watu wote: “Adhimisheni Pasaka kwa BWANA Mungu wenu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu hiki cha Agano

 

Swali: Kwa nini watoto wasishiriki Mlo wa Ushirika wa Meza ya Bwana na kwenda na wazazi wao siku hii ya usiku wa kwanza?

 

Kwenye usiku ule wa kwanza, ni wale waongofu waliobatizwa tu ambao ni watu wazima ndio wanaotakiwa waende kuhudhuria ibada hii maalumu ambayo wataiadhimisha kwa kuoshana miguu yao na kisha kuila Meza ya Bwana.

 

Yohana 13:1-17 Ilikuwa mara tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati Wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu Wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho. 2Wakati alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi Wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. 3Yesu akijua ya kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka Yake na kwamba Yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, 4hivyo aliondoka chakulani, akavua vazi Lake la nje,  kajifunga kitambaa kiunoni. 5Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi Wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni. 6Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, ‘‘Bwana, je, Wewe utaninawisha mimi miguu?’’ 7Yesu akamjibu, ‘‘Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa’’. 8Petro akamwambia, ‘‘La, Wewe hutaninawisha miguu kamwe’’. Yesu akamjibu, ‘‘Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami’’. 9Ndipo Simoni Petro akajibu, ‘‘Usininawishe miguu peke yake, bali pamoja na mikono na kichwa pia!’’ 10Yesu akamjibu, ‘‘Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.’’ 11Kwa kuwa Yeye alijua ni nani ambaye angemsaliti, ndiyo sababu akasema, ‘Si kila mmoja aliyekuwa safi.’ 12Alipomaliza kuwanawisha miguu yao, alivaa tena mavazi Yake, akarudi alikokuwa ameketi, akawauliza, ‘‘Je, mmeelewa nililowafanyia? 13Ninyi mnaniita Mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana’, hii ni sawa, maana ndivyo nilivyo. 14Kwa hiyo, ikiwa Mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. 15Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi. 16Amin, amin, nawaambia, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala anayetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. 17Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri yenu ninyi kama mkiyatenda.

 

Yesu alifanya kitendo cha kuwaosha miguu wanafunzi wake kama mfano ili kutuonyesha namna ya tabia tunazotakiwa kuwa nazo. Kitendo cha kuoshana miguu ni ishara ya unyenyekevu au kujinyenyekesha. Watu wazima wanaoshana miguu kila mtu na mwenzake kila mwaka ili kuufanya upya ubatizo wao. Baada ya kuoshana miguu ndipo tunashiriki sasa Ushirika Mtakatifu wa Meza ya Bwana, ambao unashirikishwa ama kuliwa na waongofu watu wazima na waliobatizwa peke yao. Kila mmoj anatakiwa kula kipande kidogo cha mkate usiotiwa chachu ndani yake ambao unaashiria mwili na maisha ya Yesu Kristo na kunywa kikombe kidogo cha mvinyo. Mvinyo unaashiria damu ya Yesu Kristo. Wanafanya mambo haya ili kuonyesha heshima kwa Bwana Mungu wetu kwa kuifuata Torati au Sheria zake, na kuonyesha kuwa wanamwamini nyeye peke yake.

 

Yohana 6:53-57 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.

 

Hapa Yesu anaeleza kwa nini watu wazima waongofu inawalazimu kushiriki Meza hii ya Bwana. Kama hawataila Meza ya Bwana hawataweza kuuingia Ufalme wa Mungu. Wanapaswa kujiandaa na kuwa tayari kwa kushiriki Meza ya Bwana kwa kuwasamehe wengine wenye matatizo yoyote yale ambayo yamejitokeza katika kipindi chote cha mwaka, na wanapaswa kutilia maanani pia umuhimu wa uhusiano wao na Mungu na kusahihisha makosa na kudhamiria kutotenda tena dhambi na makosa waliyoyafanywa mwaka uliopita.

 

Swali: Vihi vyakula vyenye chachu au amira ni nini?

 

Angalia jedwali letu tuliloziorodhesha picha na tangazo moja lililoorodhesha aina mbalimbali ya vyakula na vinywaji vyenye chachu na hamira. Hili litatusaidia kukumbuka na kuvijua vyakula na vinywaji vyote vyenye chachu au hamira na vile visivyokuwa navyo.

 

Pia angalia kwenye jarida la Siku Takatifu za Mungu (Na. CB22) [God’s Holy Days (No. CB22)].

q