Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 

[CB003]

 

 

 

Roho Mtakatifu ni Nini?

 

(Nakala 2.0 20021102-20061227)

 

Roho Mtakatifu ni uwezo, nguvu na mamlaka ya Mungu (a power of God). Roho Mtakatifu sio nafsi (not a person). Kwa njia ya Roho Mtakatifu tunamjua Mungu Mmoja wa Kweli na mwanae Yesu Kristo. Ni kwa njia ya Roho Mtakatifu tu, ndipo tunaweza kumjua Mungu Mmoja wa Kweli na Mwanae Yesu Kristo. Ni kwa njia ya Roho Mtakatifu tu tunaweza kufanyika kuwa wana wa Mungu kutoka katika  ufufuo wa wafu. (Kwa kuwa wote wanapoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndiyo wana wa Mungu).

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright ã 2002, 2006 Wade Cox)

(Tr. 2008)

 

 

Mafunzo haya yanaweza kunakiliwa bure na kutawanywa kwa masharti ya kwamba yatanakiliwa kama yalivyo yote bila kuongeza au kupunguzwa au kubadilishwa au kufanyiwa masahihisho. Jina la mwandishi na anwani yake na haki milki yake lazima vijumlishwe pamoja. Bila kutoza malipo yo yote wakati wa kunakili au katika usambazaji maneno mafupi yanaweza kunakiliwa katika masomo maalum na kutafakariwa bila ya kuathiri haki milki.

 

 

Mafunzo haya yanapatikana kutoka katika mtandao wa kidunia

http://www.logon.org and http://www.ccg.org

 

 


Roho Mtakatifu ni Nini?




Kuelewa Madhumuni (purpose) halisi ya Roho Mtakatifu ni lazima tumjue kwanza Mungu Mmoja wa Kweli (Eloah) na Mwanae Yesu Kristo.  Kutoka katika Biblia tutaona jinsi gani Baba na Mwana walivyo na uhusiano au wanavyounganika (Connected) katika Roho Mtakatifu (Yaani Roho Mtakatifu ndiye kiungo cha Baba na Mwana).  Tutaona ya kwamba Mungu pia huwapa Wanadamu Roho wake.  (Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake).

 

Roho siyo nafsi au kitu kilicho mbali au kilichojitenga peke yake au kilichogawanyika au kilicho mbali mbali au moja moja au kilichoachanishwa au kinachoweza kuachanishwa na Mungu Mmoja wa Kweli na Yesu Kristo Bwana hapana kabisa.  Huwezi kutenganisha Roho na Mungu au na Yesu Kristo kwa hiyo Roho siyo nafsi.

 

Wengine husema Mungu hukamilishwa katika nafsi tatu, Mwana na Roho Mtakatifu.  Hii ni Imani inayoitwa Utatu Mtakatifu (Trinity).

 

Haya si mafundisho sahihi kwa sababu tunajua ya kwamba Mungu ni MMOJA na sio watatu (Kum. 6:4; Efe. 4:6) Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu (Rum. 8:14) Mungu hutupatia Roho wake ili tuweze kumjua na kukua ili tuweze kufanana naye (2 Pet.1:3-4). Wakati mwingine Roho Mtakatifu huitwa Roho wa Utukufu au Roho wa Mungu.  Jina hili linaonyesha ni kitu kilicho KITAKATIFU au chenye Utukufu. Roho Mtakatifu hawezi kuja anatembea na kupenya kuta kutufikia sisi au akipiga makelele usiku.

 

Hatembei amejivika shuka nyeupe ili atutakase.  Anatenda kazi ndani ya mioyo yetu na katika akili zetu. Ni Jambo la kujisikia mwilini na wala si jambo la kuona kwa macho.

 

Tutapenda kutenda mambo mema na pia tutamjua Mungu anataka tutende nini yaani tutayajua mapenzi ya Mungu ndani mwetu tukiongozwa na Roho Mtakatifu. Siyo kitu cha kuogofya au kutia hofu au woga.  Mungu hakutupa Roho ya Woga, Bali ametupa Roho ya nguvu na upendo (2Tim. 1:7).

 

Roho Mtakatifu anaitwa Msaidizi (Yn. 15:26) Roho Mtakatifu anatusaidia kuielewa Biblia na mambo ya Mungu. Roho Mtakatifu anatufundisha kujua Kweli na Roho Mtakatifu ndiyo Kweli (Yn. 14:16-17,26; 16:13; 1Yoh. 4:6; 5:6) Roho Mtakatifu ndiye anajua mambo yote (KIONGOZI) (1Kor. 2:10-11) katika Roho Mtakatifu ndiyo njia ya pekee ambayo tunaweza kufanyika Wana wa Mungu.  (Yaani katika Roho Mtakatifu tunapata kufanywa kuwa Wana wa Mungu) (Gal.4:6-7; Rum. 8:14). Kristo anatusaidia, anatufundisha na kutufariji kwa njia ya kupitia katika Roho Mtakatifu.  Hii ni nguvu ya Mungu inayokaa ndani mwetu na ndani ya Kristo.  Ni kama nguvu ya uvutano inayotuvuta kwenda kwa Mungu kupitia kwa Kristo. (Ebr. 7:25) Roho Mtakatifu haonekani kwa macho.

 

Roho Mtakatifu huongea kwa niaba yetu tunapokuwa katika matatizo au shida mbalimbali (Mt. 10:20).  Hii ina maana kwamba anatufundisha kwa kuweka maneno yake katika akili zetu na katika vinywa vyetu maneno yanayositahili kusemwa ambayo sisi hatuyajui.  Mungu huwapa Roho Mtakatifu wale wamwombao (Lk.11:9-13).  Lakini ni lazima tumtii Mungu kwanza.  Roho Mtakatifu anaishi katika wale Wanaotii Amri za Mungu (1Yoh. 3:24: Mdo.5:32).

                                                                                                                                                                

Tunapoungama na kutubu dhambi zetu na kubatizwa tunampokea Roho Mtakatifu ndani mwetu. (Mt. 28:19; Mdo. 2:38) Kuonyesha mambo haya yanavyotokea, Mmoja wa Mhudumu wa Mungu anaweka mikono yake katika kichwa cha mtu aliyebatizwa na kumwombea, ili apokee nguvu za Roho Mtakatifu.  Mikono ya Mhudumu wa Mungu siyo yenye Roho Mtakatifu. Yeye ni mwanadamu na hana uwezo wake mwenyewe wa kutoa Roho Mtakatifu.  Ina maana ya kwamba yeye Anamwomba Mungu ampe mtu yule aliyebatizwa na kutubu dhambi zake, Mungu ampe Roho Mtakatifu.  Baada ya Ubatizo tunaanza safari mpya ya maisha ya kuishi katika njia ya Yesu kama yeye alivyoishi.

 

Hatupokei Roho Mtakatifu kwa kutenda tu matendo mema bali kwa kutii Sheria na Amri za Mungu hata Roho Mtakatifu anapokuwa ndani mwetu (Yak. 2:14-18).  Ukweli ni kwamba Roho Mtakatifu ndani mwetu atataka tutende matendo mema na kumtii Mungu.  Tubapokuwa hatujabatizwa kwa sababu hatujatimiza umri wa kubatizwa kwa sababu ya Uchanga wa Utoto, Roho Mtakatifu huendelea kutulinda hadi tufikie umri wa Utu Uzima na kutubu dhambi na kubatizwa kama tukiwatii wazazi na kuwaamini.  Lakini ni lazima tuwatii wazazi wetu katika Bwana (Efe. 6:1-2)

 

Kristo alisema ya kwamba alikuwa ndani ya Mungu na Mungu alikuwa ndani mwake (Yn. 17:21-23). Hii inawezekana tu katika Roho Mtakatifu wa Mungu.  Kwa hiyo tunapokuwa na Roho Mtakatifu, Mungu yu ndani mwetu na Kristo pia yu ndani mwetu (1Yoh.4:13). Hivyo ndivyo Mungu anavyohitaji kuwa juu ya yote na ndani ya yote siku moja. (Efe.4:6; 1Kor.15:28) Lakini katika wakati huo wote tutakuwa katika hali ya maumbile ya Kiroho na hatutakuwa tena katika miili ya nyama na damu ya kibinadamu.

 

Roho Mtakatifu ndiyo KIUNGO kinachotuunga wote pamoja. Kumbuka, Roho Mtakatifu sio kitu cha kusikia au kugusa kwa mikono.  Tunamtambua Roho Mtakatifu kuwa yupo au haupo kutokana na yale yaliyomo ndani ya akili zetu na jinsi tunavyoenenda.  Mienendo yetu, jinsi tunavyotenda ndiyo kipimo cha kuwa na Roho Mtakatifu au kutokuwa na Roho Mtakatifu (Gal. 5:16-18).

 

Kama Wakristo tunapaswa kuishi katika njia aliyoishi Kristo na katika njia walioishi Mitume.  Tunajua waliitunza Sabato na Sikukuu Takatifu (Matendo 2:1, 20:6; 27:9; Kol. 2:16). Kujua na kufahamu ni nini Mungu anachosema ndani ya Biblia. Hakutoshi kutufanya kupata kubadilika bila ya kuyatenda yale yaliyoandikwa.  Ni lazima tutende yale yote Mungu aliyoyaamru.  Tunapokuwa na Roho wa Mungu na kuishi katika njia aliyoiamru Mungu, tunaanza kuonyesha matunda ya Roho Mtakatifu katika matendo yetu ya kila siku tunayotenda na katika maisha yetu ya kila siku tunayoishi. Tunaweza kusoma juu ya haya yote katika (Wagalatia 5:22-23.)  Upendo ndiyo tunda kuu la Roho, lakini yote yanaanza kwa kuitambua na kuiamini Kweli (1Kor. 13:13).

 

Kuwa na Roho ina maana tunaweza kuongea na Mungu katika Maombi.  Tunapoomba lazima daima tuombe mahitaji yetu katika jina la Mwanae Yesu Kristo (Mt.6:6, 9-13; Lk.11:12).  Kwa hiyo tunasema na Baba kupitia kwa Mwanae.  Hii ina maana ya kwamba Yesu ni kama mwanadamu aliye katikati.  Kama hatujui namna ya kuomba kama inavyostahili, Roho Mtakatifu Mwenyewe hutusaidia katika udhaifu wetu na hutuombea kwa niaba yetu kama Baba apendavyo.

 

Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa (Rum. 8:26).  Mungu daima anajua mawazo yaliyomo katika mioyo yetu na yote tunayowaza akilini mwetu. Kwa hiyo Mungu anajua mahitaji yetu ambayo Roho anatuombea kwa niaba yetu.  Roho huwaombea Watakatifu kama apendavyo Mungu (Rum. 8:27).

 

Kristo ni mfano wa jinsi gani alivyo Baba.  Alitenda na kuzungumza kwa niaba ya Mungu (Yn. 3:34). Kwa sasabu ana Roho Mtakatifu wa Mungu anayekaa ndani yake.  Lakini Yeye siyo sawa na Mungu Mmoja wa Kweli, Yuko mbali na aliumbwa na Mungu na kutumwa hapa duniani kama Mwanadamu kwa muda mfupi (Yn. 5:23). Wote Baba na Mwana wako mbali lakini ni Umoja kwa sababu wanashirikiana katika asili ya maumbile kuwa sawa (the same nature) katika Roho Mtakatifu Kristo alisema “Ukiniona mimi basi, umemwona Baba” (Yn.14:9).

 

Mungu hawezi kutenda dhambi, lakini Kristo anaweza.  Kristo alijaribiwa kutenda makosa, lakini alichagua kutotenda kosa, kwa sababu alikuwa anamtii Mungu wake ambaye ni Baba yake (Mt.4:1-11).  Aliweza kuyashinda majaribu ambayo yangeweza kumletea dhambi kwa sababu alipata nguvu kupitia katika Roho Mtakatifu.

 

Roho Mtakatifu hutuunganisha wote kwa pamoja na kuwa Hekalu la Mungu. (1Kor. 3:16; 6:19). Mungu anatuita katika ufalme wa Mungu ili tuweze kutenda kazi pamoja.  Roho Mtakatifu hutupatia sisi sote vipawa maalum au hutujalia ili tuweze kutenda kazi pamoja kila mtu akiwa kiungo kwa mwenzake.  Mtu mmoja hawezi kujaliwa vipawa vyote. Kwa hiyo tunahitaji kusaidiana wote kila moja na mwenzake katika kazi ya ujenzi wa Kanisa kwa Upendo na katika nguvu za Roho Mtakatifu.

 

Hatuwezi kuingia katika Ufalme wa Mungu bila kuzaliwa mara ya pili.  Hii inatokea pale tunapobatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu.  Ndipo tunapozaliwa na Roho na matendo mafu yetu ya zamani yanakuwa yamekufa (Yn.3:3-6)  Wale walio wa matendo ya kimwili hawawezi kumfurahisha Mungu. Kwa hiyo tunapokuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu tunakuwa na Kristo anaishi ndani mwetu na Mungu  pia ndani mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu (Rum.8:8-10). Kwa hiyo Roho Mtakatifu anatufundisha na kutupa maisha mapya.  Ingawa bado tuko katika umbo la kibinadamu (Kimwili) hatuishi tena katika njia ile ambayo watu wengi wa dunia hii wanaishi, bali lazima tubadilike na kuishi katika maisha mapya katika Kristo (Efe. 4:17-24).

 

Watu wengi hawatii Sheria na Amri za Mungu.  Badala yake wanasherekea sikukuu za kipagani na kuwaabudu miungu ya uongo.  Lakini wamedanganywa na Shetani na Mungu bado hajawafunulia kuyajua Mambo ya Mungu.  Kwa hiyo sio makosa yao hasa na Mungu bado hajawahukumu.  Tuliacha njia hii ya kuishi katika maisha kama haya pale tulipoungama dhambi zetu na kutubu na kubatizwa Hatuwezi kurudi tena katika maisha hayo tena.

 

Roho Mtakatifu hutuacha tunapotenda dhambi (1The. 5:1; Efe. 4:30).  Tunapopokea Roho ndipo tunapomjua Mungu zaidi na mpango wake wa wokovu kwetu.  Lakini tukirudia dhambi tena yale mambo yote ya ajabu na ya Siri za Mungu tulizopata kufahamu zinapotea zote mara moja (2Tim.1.14) Tunapofikiria na kutenda mambo yale ambayo hayampendezi Mungu, hapo tunaelewa wazi ya kwamba Roho Mtakatifu ametutoka na kutuacha peke etu.  Mungu akasema hatatupungukia wala kutuacha (Kum. 31:8; 1Fal. 6:13; Isa. 42:16; Ebr.13:5). Lakini Roho anaweza kuzimwa au kuhuzishwa (1The 5:19; Ef. 4:30). Tunamwabudu Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu (Flp. 3:3). Kwa hiyo Roho Mtakatifu sio Mungu na hatumwabudu Roho Mtakatifu.Wala hatumwabudu Yesu Kristo. Kama tunajua ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu yuko ndani mwetu na sisi tumo ndani Mwake katika Roho Mtakatifu wake (1Yn. 4:15).

 

Watu wa Agano la Kale pia walijua juu ya Roho wa Mungu.  Walishuhudiwa na kuwapo kwa Malaika wa Yehova.  Walijua hakuwa Mungu Mmoja wa Kweli aliyekuwa akisema nao, na yule waliyemwona, kama tunavyojua ya kwamba kuwepo kwa huyu Malaika wa Mungu ambaye alikuwa na Musa na Wana wa Israeli kule Jangwani ndiye alizaliwa kama mtu Mwanadamu Yesu (Angalia somo la Yesu ni nani? (CB002)).

 

Manabii wote walitembelewa na Roho wa Mungu katika ndoto au katika maono. Roho ambaye alikuwa akipitia kwa Malaika wa Yehova.  Bwana alikuja kwa Ibrahim katika maono (Mwa. 15:1). Bwana alimwita Haruni na Miriamu (Hes.12:6).

 

Roho wa Mungu Ikamjia Balaamu (Hes. 24:2), Bwana akamwita Samweli (1Sam. Sara ya 3), Isaya aliona Maono (Isa. 1:1) Neno la Mungu likamjia Yeremia (Yer.14:14), Ezekieli aliona Maono ya Mungu (Eze.1:1).

 

Danieli alipewa maono (Dan. 2:19) kadhalika ilikuwa kwa Manabii wote wa zamani.  Biblia inazungumzia Roho ya mwanadamu ni tofauti na Roho wa Mungu.  Ni sawa na pumzi. Ni kipawa cha uzima kutoka kwa Mungu (Zek. 12:1).  Ni ya Mungu (Mwa. 6:3; Ayu. 11:11; 27:3; Mit. 20:27).  Tunapokufa Roho wa Mwanadamu hutuacha (Zab. 146:4). Inamrudia Mungu (Mhu. 12:7).  Mungu alipomwuumba Adamu alimpulizia puani pumzi ya Uhai, na mtu akawa nafsi hai (Mwa. 2:7; 1Kor. 15:45).

 

Kwa hiyo Roho hii iliyoko ndani ya mwanadamu sio nafsi inayoishi mbinguni tunapokufa. Biblia inasema mwanadamu akawa nafsi hai au mtu.  Nafsi hii inaweza kufa (Eze.20:18). Biblia inapozungumzia kuhusu nafsi inazungumzia hasa maisha ya mwili.  Nafsi ina maana ya kiumbe, au mtu au maisha. Wote wanyama na wanadamu wanakufa kifo kimoja, lakini Mwanadamu ataishi tena (Yaani baada ya ufufuo).

 

Kwa hiyo Roho iliyoko katika Mwili wa Mwanadamu ndiyo inayotofautisha baina ya wanadamu na wanyama. Kwa hiyo Roho ya Mwanadamu haiwezi kuonekana kwa macho zaidi  tunavyoweza kuiona pumzi yetu, lakini tunaweza kusikia pumzi yetu.

 

Kama vile tusivyoweza kuona Roho wa Mungu, Lakini tunasikia kuwepo kwake ndani mwetu, kwa sababu tunahitaji kumtii Mungu.  Roho wa Mungu ni sawa sawa na upepo (Yn.3:8). Kwa namna nyingine ni sawa na pumzi.

 

Yesu alipokufa juu ya mti alimwita Baba yake kutoka Mbinguni, Baba mikononi mwako naiweka Roho yangu.  Alipokwisha kusema hayo alipumua pumzi ya Mwisho akakata Roho (Lk.23:46).  Kwa hiyo ndiyo Roho ambayo Wanadamu wote wanayo, ambayo inamrudia Mungu wakati wa kufa.  Aliweka maisha yake mikononi mwa Baba yake.

 

Yesu alijua ya kwamba iwapo ataendelea kushi tena baada ya kifo cha kibinadamu.  Ni Baba yake tu ambaye angewezana tena kumpa maisha mapya.  Kwa hiyo katika Roho Mtakatifu Mungu alimfufua Yesu kutoka katika mauti (Mdo. 2:32,33). Kwa njia hiyo hiyo alivyomfufua Mwanae nasi pia tutafufuliwa kutoka katika wafu ili tuweze kuishi tena katika maisha mapya (Rum. 8:11).

 

Yesu alipokuwa duniani alijazwa na nguvu za Roho Mtakatifu.  Kwa hiyo kwa sababu aliongozwa na Roho Mtakatifu alitenda yale ambayo Baba alimwagiza ayatende (Lk. 2:49).  Kristo alisema ya kwamba asingeweza kutenda jambo lolote mwenyewe bila ya Baba.  (Yn. 5:30).  Aliwafundisha wanafunzi wake mambo mengi juu ya Mungu na juu ya mambo yatakavyotokea au kuwako mbeleni (Yaani mambo ambayo yatatokea baadaye).  Alikuwa kama uwepo wa Mungu kwa sababu alizungumza kwa niaba ya Mungu.  Alikuwa na akili sana na alitenda miujiza kupambanua mafundisho kwa wanafunzi wake.

 

Lakini bila ya Roho Mtakatifu wasingeweza kuelewa.  Roho Mtakatifu ni uweza na nguvu ya Mungu, ambao Kristo alioahidi kutuletea (Yn.16:7). Kabla ya Yesu kuwaacha Wanafunzi wake akiwa katika hatua za mwisho za kurudi kwa Baba yake mbinguni (Mdo..1:10-11) aliwaagiza wanafunzi wake wasitoke Yerusalemu, Lakini wasubiri ahadi ya Baba.  Aliomba kwa Baba kuwapa Msaidizi mwingine (Yn. 14:16-17).  Aliwaambia ya kwamba watapokea Roho Mtakatifu kutoka kwa Baba (Yn. 15:26).  Hii ilimaanisha ya kwamba bado alikuwa yuko pamoja nao katika Roho Mtakatifu ambaye watampokea baadaye kama yeye alivyompokea.

 

Kwa hiyo walipokuwa wamekusanyika wote mahali pamoja katika sikukuu ya Pentekoste,  tukio kuu la ajabu lilitokea.Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi.  Kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliokuwa wameketi.  Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.  Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka (Mdo. 2:1-4). Hii ilikuwa ni ishara ya nguvu walioipokea kama alivyoahidi, lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu. Moto haukuweza kuwadhuru.

 

Roho Mtakatifu atawafundisha yote na kuwakumbusha yote na mambo ya mbeleni atawapasheni kama vile Kristo alivyofanya wakati alipokuwa nao katika nafsi (Yn. 14:26). Katika Roho Mtakatifu Kristo atawasaidia na kuwaimarisha na kuwatia nguvu, katika Imani na kujenga Kanisa la Mungu.  Sasa tutaendelea na kazi hii mpaka hapo Kristo atakaporudi tena na kuiweka Sayari hii katika hali ya ukamilifu kama mwanzo mbapo tutakuwa tunatii Sheria na amri za Mungu.

q