[CB001]
Mungu ni Nani?
(Nakala 3.
020020725200505062006122720070712)
Mungu (Eloah) wa pekee Mmoja ndiye Mungu wa kweli. Kabla yake Mungu hakuumbwa awaye yote, wala baada yake hatakuwepo yeyote mwingine. (Isa. 43:10) masomo haya yanayolenga katika kutufundisha kumjua Mungu yakijikita zaidi katika kutufundisha jinsi tunavyoweza kumjua Mungu,na Kunyenyekea kwa Kicho Kwake na Kumwabudu yeye Mungu Mmoja wa Kweli wa pekee.
Christian
Churches of God
Barua Pepe:: secretary@ccg.org
(Haki milki © 2002 2005, 2006,2007, CCG,
ed. Wade Cox)
(Tr. 2008)
Mafunzo haya yanaweza kunakiliwa bure na kutawanywa kwa masharti ya kwamba yatanakiliwa kama yalivyo yote bila kuongeza au kupunguzwa au kubadilishwa au kufanyiwa masahihisho. Jina la mwandishi na anwani yake na haki milki yake lazima vijumlishwe pamoja. Bila kutoza malipo yo yote wakati wa kunakili au katika usambazaji maneno mafupi yanaweza kunakiliwa katika masomo maalum na kutafakariwa bila ya kuathiri haki milki.
Mafunzo haya yanapatikana
kutoka katika mtandao wa kidunia
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mungu ni Nani?
Siliza, Ee Israeli, BWANA, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja! (Kum. 6: 4).
Ni dhana iliyodhahiri na wazi kutoka katika Biblia inayodhihirisha ya kwamba kuna Mungu mmoja tu wa kweli. Mungu (Eloah) ni Alpha na Yeye ni Omega
Mwenyezi Mungu, Mwenye Enzi, Mwenye Nguvu zote, Mweza wa yote na Muumbaji wa Mbingu na vyote vilivyomo. (Mwa.1:1; Neh. 9:6; Zab.124:8; Isa. 40:26,28; 44:24; Mdo14:15; 17:24,25; Ufu.14:7)
Kulikuwa na wakati ambapo hakuna kitu cho chote kilicho ishi, yaani nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, ila Roho wa Mungu aliyekuwa Mmoja. Alikuwako tangu milele. Tangu mwanzo, alikuwako Yeye wa Pekee, hakuhitaji kitu cho chote ili kupata Nguvu au Uhai. Huyu ndiye Mungu Mmoja na wa Kweli. (Yn. 17:3:1Yon. 5:20) Ni Mungu wa Milele (1Tim 6:16). Hii ina maana ya kwamba ni Mungu asiyekufa. (Mungu asiyepatikana na mauti)
Mithali 30:4-5 inaonyesha jina la Mungu ya kwamba ana Mwana.
Ni nani aliyepanda Mbinguni na kushuka chini?
Ni nani aliyekamata upepo kwa mokonzi yake?
Ni nani aliye yafunga maji ndani ya nguo yake?
Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi?
Jina lake ni nani? Na ni nani jina la Mwanawe, kama wajua?
5. Kila neno la Mungu limehakikishwa: Yeye ni
ngao yao wamwaminio.
6. Usiongeze neno katika maneno yake; Asije
akakulaumu, ukaonekana u mwongo (NIV)
Hapo mwanzo Mungu (Eloah) alianza Uumbaji. Lakini kabla ya kuanza Uumbaji wa cho chote, Mungu alijua ni nini atakachokiumba na kwa namna gani atakavyoumba. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Alijua hata mwisho wa uumbaji wake wa kila kitu. Kwa kila kitu ambacho kilitokea kuwepo, Mungu (Eloah) alijua jinsi ya utendaji wa kazi wa kila kiumbe katika uumbaji na uhusiano kati ya kila kimoja na kingine.
Mungu (Eloah) ni Alpha na yeye ni
Omega (Uf.1:8) Yeye ni wa
Pekee alikuwako tangu Mwanzo na
wa Milele, kwa hiyo ni Alpha, au Mwanzo. Yeye ni Omega
kwa sababu yeye atakuwa wa
mwisho katika vyote alivyo viumba.
Uumbaji unaendelea kwa sababu ya
Yeye. Uumbaji umejikita juu Yake na Yeye Ndiye yote katika wote. Kwa hiyo Mungu mwenyewe anajipanua katika dhana ya uumbaji
Kwa mwanadamu (kutoka 3:14)
Mungu akawa Baba alipoumba familia kwa ajili yake. Lakini tutajifunza zaidi juu ya familia ya Mungu katika
somo la Uumbaji
wa Familia ya Mungu (Na. CB004).
Kabla ya kitu cho chote kuwepo,
Mungu alijua atakacho kiumba na kwa namna
gani. Alijua kila kitu kitakavyokuwa.
Alijua kabla, matokeo na mwisho
wa kila kitu.
Hakuna cho chote kilichofichika au kilichofanyika kwa siri ambacho
Mungu hakukijua kabla ya Uumbaji
kuanza. Mungu alijua kila kitu
(1Yoh. 3:20). Tendo hili la Mungu
kujua kila kitu yaani kujua
yote linaitwa hekima kuu ya Mungu
(Omniscience). Mungu hakutaka
msaada wa kitu cho chote,
kutoka kwa ye yote kumsaidia yeye katika kufikiri, kufanya maandalio, au kufanya hesabu kabla ya uumbaji.
Aliweza yeye mwenyewe kufikiri na kufanya hesabu
ya kila umbo na aliweza
kuona ni njia ipi ambayo
kila chaguo lake lingeweza kutekelezwa.
Mungu ni Mweza wa yote. (Mwenye Nguvu na Mamlaka).
Hakuna kitu ambacho hawezi kukifanya kikamilifu kutimiza mapenzi ya mpango
wake. Yeye anajua yote yanawezekana
kwake, na anajua njia sahihi
ya kuumba vitu mbalimbali.Kila kitu kilichoumbwa kiliandaliwa na kuthibitishwa, kudhihirika tangu mwanzo. Huo ni pamoja na
Uumbaji wetu sisi. Kila kitu kilionyesha maana katika kutenda kazi njema hata
mwisho.
Mungu alijua ni jinsi gani vitu vingeweza kutengenezwa, na kwa namna gani na kwa idadi gani na kadhalika. Elimu hii ni kweli; Mungu ni Kweli (Kum 32:4). Mungu aliweza kuumba ulimwengu na vitu vyote bila kubahatisha au kujutia matokeo yake. Kwa hiyo, mapenzi yae yalileta nuru ya utimilifu wake katika ukweli (Mungu ni Kweli) Kwa asili au kitabia Yeye hana makosa yo yote (Yaani ni Mkamilifu Mtakatifu na kazi yake haina makosa kiasili na kitabia) Mungu hawezi kutenda kosa kwa sababu ya uweza na uhodari wake mkubwa katika utendaji wake. Humuwezesha kuepukana na majuto katika hekima yake kuu ya kujua yote, inamfanya Mungu kuwa Mkamilifu (Mt. 5:48).
Kabla ya kuanza Uumbaji, Mungu alijua ya kwamba kazi yake yote itakuwa kamilifu na njema. Alijua ni nini kilichokuwa chema sana, kwa sababu Mungu alipenda Uumbaji uwe kama yeye Mwenyewe na kuwa Nuru kama yeye Mwenyewe alivyo nuru. Mapenzi ya mwisho ya Mungu ni wema (Zab. 25:8) Chanzo cha wema wote hutoka kwake. Wema wote hutoka kwake. Mtu mmoja aliposema yakuwa Kristo ndiye Mwalimu Mwema, Yesu alijibu, kwa nini unaniita Mimi Mwema? Mungu tu ndiye Mwema (Mt. 19:17; Mk. 10:18, Lk. 18:19).
Mungu ni Upendo (1Yoh. 4:8; Rum. 13:10) Sio Mungu wa kuadhibu katika mateso ya milele ambayo wengine wanamfanya yeye kuwa hivyo. Ni Mungu wa msamaha na rehema. Hata alitayarisha toba kwa Shetani na kwa wale walioanguka. Mungu anataka mema kwa kila mtu. Mara Uumbaji wa dunia itakapokamilika katika Mapenzi yake ya Mamlaka yake katika Nguvu za Kiroho kila mwana na binti wa Adamu watakuwa wamoja kama watoto wa Mungu.
Mwisho wa mambo yote, wote tutajua na kuishi katika maisha ya ukamilifu ya Upendo kati ya mtu na mtu na kuona jinsi Mungu wa Ajabu wa Kweli alivyo, na Yeye tunapopendana na jirani zetu inadhihirisha utimilfu wa Upendo wa Mungu kati yetu (1Yoh. 4:20-21) mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na Ndugu yake, kaka yake na dada yake (NCV)
Mungu anatuhitaji sisi wote tuwe watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu (Kut. 22:31; Law. 11:45; 19:2; 20:7; 21:8). Hatua hii inaweza kufikiwa iwapo tutaishi kwa kuitazama sheria kamilifu ya Mungu iliyo ya uhuru na kukaa humo (Yak. 1:25)
1Petro 1:14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na temaaa zenu za kwanza za ujinga wenu;
15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo Mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 Kwa maana imeandikwa, Mtakuwa Watakatifu kwa kuwa Mimi ni Mtakatifu (NCV).
Mungu ametupa sheria na Amri zake, ambazo ni Nuru ya tabia yake mwenyewe; Ni Takatifu, za haki na njema kama yeye mwenyewe alivyo Mwema (Rum.7:12) kutotii Sheria na Amri za Mungu ni kwenda nje na tabia ya Mungu. Mungu anapenda Sheria na Amri zake ziandikwe ndani ya mioyo yetu. Kristo alituonyesha jinsi gani tunavyoweza kupendana kati ya mtu na mtu kwa kutii Amri za Mungu. Aliishi katika maisha yasiyokuwa na dhambi, Mnyenyekevu Yeye mwenyewe mbele ya Mungu wake na Aliutoa Uhai wake kwa ajili yetu sisi wote; ili na sisi pia tuweze kuwa na Upendo wa Mungu na kwa hao ndugu zetu kama alivyotupenda sisi. Mungu anatuhitaji tuenende katika mfano wa Mwanawe Yesu Kristo (Rum. 8:29; 1kor. 11:1).
Hakuna mtu aliyemwona
Mungu au kuisikia sauti yake (Yn. 1:18; 5:37). Manabii wa zamani
hawakumwona au kumsikia Mungu au Eloah; badala yake, waliona na
kusikia malaika wa Yehova ambaye
baadaye alikuwa Yesu Kristo
(Angalia somo la Yesu ni
Nani? (Na. CB2)).
Jinsi gani tunavyoweza
Kuujua Ukuu na Uweza wa
Mungu kuwa Yuko na Yu Hai?
Imeandikwa kwamba ni mpumbavu tu anayeweza kusema moyoni mwaka ya kwamba hakuna Mungu (zab. 14:1) Mungu (Eloah) alikuwako tangu mwanzo, Yuko, na Yu hai milele. (Zab. 93:2). Mungu ni Roho.
Yohana 4:24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa Kumwabudu katika Roho na Kweli (NIV)
Mungu amethibitisha kuwako kwake kwa kazi Zake nyingi, Aliumba Mbingu na Nchi (Mwa.1:1). Mungu ( Eloah) ni Muumbaji wa kila kitu (Ebr. 3:4 ) kila kitu ni mali yake (1Nya. 26:16). Ni Mungu (Eloah) aliyetuumba na sisi ni mali yake. Sisi ni watu wake, kondoo wa malisho yake (zab. 100:3).
Yesu alikuja kutufundisha juu ya kumjua Baba.
Yohana 7:28 Basi Yesu akapaza sauti yake Hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua, wala sikuja kwa Nafsi yangu; ila Yeye aliyenipeleka ni wa Kweli, msiyemjua ninyi. (RSV).
Kwa Kuwa ni
Kweli Kwamba Tunaugua na
Kufa, Je, Inamaanisha Ya Kwamba Mungu
Hatupendi?
La hasha (hapana) matatizo mengi ya mwanadamu yanasababishwa na kutokutii sheria na amri za Mungu kula vyakula najisi vinaleta madhara ndani ya miili yetu. Wanadamu wengi hawafuati kanuni za afya na kinga kwa hiyo husababisha kuenea kwa wadudu waenezao magonjwa kutoka mtu hadi mtu. Wanadamu wanaendelea kuwa dhaifu na dhaifu katika makundi kwa sababu ya kizazi kikaidi kisichotii. Sheria na amri za Mungu. Pia, hatuitunzi vizuri ardhi kama Mungu alivyotuagiza. Vita vinaleta madhara mengi na hii sio kazi ya Mungu. Wanadamu wanadhulumiana mtu na mtu, na kuoneana na wengine wanajiharibu miili yao wenyewe. Tunachafua Ardhi pia, kwa hiyo sisi wenyewe nduyo wahusika wakuu na chanzo cha madhara yanayotupata (Angalia somo la Sheria za vyakula za kibiblia (NA. CB19)).
Je, Mungu
Kweli Anajali Yanayompata Mwanadamu?
Ndiyo Mungu anatujali sana. Mungu anatujali na anatupenda kwa upendo Mkuu. Mungu hataki kitu chochote kiingilie kati yetu na Yeye. Mungu anahitaji sisi tumjue na kumfahamu ya kwamba hakuna ye yote anayelingana na Mungu katika Nguvu na Uweza wake (Kum. 4:35). Mungu alimpa mwanadamu mwanzo Mkamilifu (Mwa. 1.26-30). Lakini Mwandamu aliikataa sheria na amri za Mungu na kuamua kutenda mambo kama apendavyo mwanadamu mwenyewe (Yaani mwanadamu alikakataa njia ya Mungu na kuamua kufuata njia yake mwenyewe) Hii imeleta taabu kubwa ya matatizo mengi juu yetu (Rum. 5:12). Kumbuka Mungu alimtuma Mwanawe kwa ajili ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu kutoka katika dhambi na Mauti. Huu ni udhihirisho wa Upendo wa Mungu kwa Wanadamu (Yn. 3:16).
Tusikate tamaa wakati mambo yana kwenda vibaya. Hatuwezi kuuliza, Mungu yuko wapi? Kwa nini mambo haya yametokea kwangu? Mungu anajua kila jambo linalotokea katika maisha yetu. Kumbuka, Yesu alikamilishwa katika mateso. Na sisi pia lazima tutegemee kujifunza kutokana na majaribu na mateso yanayotupata. Lakini Mungu hawi mbali nasi. Hawezi kuruhusu tubebe mizigo ya matatizo na mateso inayo weza kuzidi uwezo wetu wa kuvumilia. Lazima tufurahi mioyoni mwetu Kwa kuwa tunamwamini Mungu (Zab. 33:20 21) Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; Lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (1Kor. 10:13)
Imetupasa Kuomba Kwa Nani?
Wanafunzi wa Yesu walimwomba awafundishe kuomba (Lk.
11:1). Yesu kisha
akawapa mifano fulani namna ya
kuomba na waombe kwa nani.
Soma maandiko na ugundue ya kwamba maombi yameelekezwa kwa Baba peke yake.
Mathayo 6:6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye Sirini, na Baba yako aonaye sirini atakujazi (RSVC)
Kisha Yesu akafuatisha namna ya kuomba (Mt. 6: 9-13) Angalia Msitari wa 9:
Mathayo 6:9 Basi ninyi salini hivi: Baba yetu uliye Mbinguni, Jina lako litukuzwe, (NIV)
Kama Wakristo ni lazima tufuate nyayo za Yesu Kristo. Kwa hiyo tunapoomba tunaomba Kwa jina lake Bwana Yesu Kikristo.
Yohana 14:13-14 Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana 14. Mkiomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya (RSV)
(Angalia pia Yn. 15:7)
Mungu anatusikia sisi kutoka mbinguni.
Bwana Mungu huwasikia na kuwakubali wale Wanaomnyenyekea kwa Kicho. Mungu hatawasahau. (Wanaomnyenyekea na kumwogopa na kutetemeka mbele ya Mungu) (Mal.3:16) Tunapoomba lazaima tutoe shukrani kwa Mungu kwa ajili ya Mibaraka yake Mingi na kwa maajabu ya uumbaji wake aliotuonyesha (zab. 105:1)
Kwa habari zaidi angalia Somo
la maombi sehemu A mwongozo wa mwalimu
(CB31) na Somo
la maombi sehemu B karatasi ya maandalio
(CB32).
Je ni Muhimu
Kuchangua Mungu wa kumwabudu?
Ndiyo ni muhimu sana kwamba tumwambudu anayeisitahili kuabudiwa. Lazima tumwabudu Bwana Mungu wetu mbele zake (Kum. 26:10; ISam.1:3; 15:25). Lakini Mungu huyu ana nafsi mbili au ni wa nafsi tatu? Ha-hasha! (Hapana) tunaweza kusema ya kwamba Yesu Kristo Mwana wa Mungu ni Mungu kama Mungu alivyo Mungu Baba? Jibu ni wazi kwamba La hasha (Hapana).
Yesu anazungumzwa kama Mungu (Yn 1:1). Hata kama Mungu mwenye nguvu (uwezo) mwingi (Isa. 9:6). Lakini hakuna mahali ambapo anasemwe ni Mungu mwenyezi (Mwa. 17:1). Yesu hakuna mahali popote anapojipandisha katika nafasi ya Baba yake. (Lk. 4:8) Yesu ni Mungu, lakini sio yule Mungu Mmoja wa kweli. Yeye ni nafsi ya Kiroho, lakini kwa sababu ya kutii kwake ni Umoja na Baba.
Yesu anatwambia ya kwamba mapenzi ya kuabudu kwetu ni kwa Baba na sio kwake, (Mungu Mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote).
Yohana 4:23. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho na kweli, kwa maana Baba awatafuta awatu kama hao wamwabudu. (NIV)
Ni Wakati Gani
Tumwabudu Mungu Wetu?
Mungu Mmoja wa kweli ametupa kalenda na maelekezo maalum
katika siku ambazo ni Takatifu na
zinapaswa kuangaliwa ili katika siku hizo watu waweze
kusanyika kwa pamoja na kumtukuza
Mungu. Nyakati hizo na siku hizo
Takatifu zimeelezwa zote katika masomo
yafuatayo: Kalenda takatifu
ya Mungu Na. CB 20: siku ya Sabato (Na. CB21); siku takatifu
za Mungu (Na. CB22).
Hapana mwingine mfano wa Mungu
Baba (kut. 8:10) Mtukufu katika Utakatifu, mwenye kuogopwa katika sifa, mfanya
maajabu (Kut. 15:11).
Isaya 44:6 BWANA, Mfalme wa Israeli, mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na Mimi ni wa Mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu(RSV)
Mtume Paulo aliwaandikia wakristo wa kweli;
1Wakorintho 8:5-6 kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; 6 lakini kwetu sisi Mungu ni Mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, Yuko na Bwana Mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwepo, na sisi kwa yeye huyu tunaishi (NIV)
Hapana mwingine yeyote awezaye kuitwa katika Jina hili la Mwenyezi Mungu (Eloah, kwa Kiebrania). Ibada zote za kuabudu sanamu watakatifu waliokufa, Bikira mariamu na shetani ni miungu ya uongo.
Hatupaswi kuabudu mingu mingine yo yote (elohim) zaidi ya Mungu ambaye ni Baba (Kut. 34:14; Kum. 11:16) au vinginevyo tutangamia (Kum. 30:17-18). Mungu alitupa Amri yake ya kwamza isemayo:
Kut. 20:2 Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi utumwa, usiwe na miungu mingine (elohim) ila Mimi tu (NIV).
Mungu (Eloah) ni Mungu wetu na Baba na Mungu na Baba yake Yesu Kristo (Yn. 20:17) Mungu alituumba sisi wote na tuna Baba mmmoja tu (mal. 2:10) Mungu wetu ambaye yuko Mbimbuni (mt 23:9). Yeye ni Mungu Mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote (Efe. 4:6)
Kuna Mungu (Eloah) wa Kweli Mmoja tu. miungu (elohim) mingine yote ipo kwa sababu ya mapenzi yake. Inaendelea kuwepo kwa sababu ya kutii mamlaka ya Mungu (eloah).
BWANA MUNGU
Anafadhili, ni mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema. Amejaa upendo (Zab. 145:8:34:6) kila wakati anatupenda na yupo kwa ajili ya kutusaidia katika shida zetu zote (Zab. 46:1) Mungu anatuhitaji sisi wote tuwe kama yeye. Kila mtu anayezaliwa wakati wo wote anayo nafasi ya kupokea uzima wa Milele. Mapenzi ya Mungu ni kwamba watu wote wachague kuishi katika Amri zake.
Jinsi tutakavyozidi kumjua Mungu ni nani
na kuanza kuishi katika njia
zake, hapo ndipo tutakapoona ya kwamba njia
zake ni sahihi
na kamilifu na njema sana kama
ukiichagua, hutajuta. Tunavyozidi kusoma na kujifunza neno
lake ndipo tunapozidi kugundua ya kwamba
neno lake ni kamili na timilifu
yaani neno la Mungu halina makosa.
Kwa hiyo kama tukimwamini Mungu na kumtii atatulinda
na kutuhifadhi. (Zab.
18:30; Mit. 30:5). Lazima tumjue tumwamini na kumwabudu Mungu
Mmoja wa kweli kabla hatujajua siri za Mungu. Hii inachukua muda lakini tunayo nafasi
ya pekee ya ajabu katika
maisha yetu ya mbeleni.
Na mwisho wa mwanadamu ni kuwa kama mungu (Elohim) kama Yesu Kristo aliyekuwa malaika wa Bwana katika Agano la kale (Zek. 12:8)
q